KWELI Fanz Riechelt alifariki alipokuwa wakati akivanya majaribio ya uvumbuzi wake wa Parachuti

KWELI Fanz Riechelt alifariki alipokuwa wakati akivanya majaribio ya uvumbuzi wake wa Parachuti

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mnamo mwaka 1912, mvumbuzi na fundi nguo Franz Reichelt alipoteza maisha baada ya kuruka kutoka Mnara wa Eiffel nchini Ufaransa akijaribu kuvumbua vazi la parachuti aliloamini lingeweza kumnusuru mtu anayeanguka kutoka juu. Jaribio hilo lilifanyika mbele ya mashuhuda na kurekodiwa kwa kamera, lakini kifaa hicho hakikufunguka kama alivyotarajia na kusababisha kifo chake papo hapo.

Zaidi ya karne moja baadaye, tukio hilo linaendelea kuzua mijadala kuhusu mipaka ya ubunifu, ujasiri na hatari katika sayansi na teknolojia. Wapo wanaomwona Reichelt kama mtu aliyekuwa mbele ya wakati wake na aliyetoa mchango kwa maendeleo ya usalama wa anga, huku wengine wakiamini alichukua hatari kubwa isiyo ya lazima. Wewe una maoni gani—je, alikuwa shujaa wa uvumbuzi au alipaswa kutathmini hatari kwa umakini zaidi?

IMG_4993.jpeg
 
Tunachokijua
Kati ya mwaka 1910 hadi 1912 mbunifu wa mavazi raia wa Austria Fanz Riechelt aliamua kubuni vazi (suti) itakayokuwa na uwezo wa kutumika kama parachuti kwa marubani ili kujiokoa wanapopata changamoto.

Katika majiribio yake kadhaa Fanz alitumia midoli kwa ajili ya majaribio kwa kuivalisha midoli hiyo na kuitupa kwa kupitia dirishani katika makazi yake, lakini baada ya muda akaona kuwa anahitaji eneo refu zaidi.

Aliamini eneo refu zaidi litampatia uwezo wa kuona uwezo wa vazi hilo kwa kuirsha midoli yake katika umbali mrefu zaidi na ndipo alipoomba kibali cha kutumia mnara wa Eiffel uliokuwa na urefu wa futi 187 mara tano zaidi ya maeno aliyokuwa akiyatumia awali.

Februari 4, 1912 alienda kufanya majaribio yake katika mnara huo, lakini mamlaka walijua atatumia midoli yake kama ilivyo kawaida lakini ghafla wakamuona anajirusha mwenyewe akiwa na vazi lake na kwa isivyo bahati halikufanya kazi vizuri.

Hatimaye, Franz Reichelt ameungana na watu wengine wengi waliopoteza maisha wakitafuta njia salama ya kurusha binadamu angani. Kwa upande mmoja, ujasiri wake na imani yake kwa uvumbuzi wake vinastahili kutambuliwa, lakini kwa upande mwingine, uamuzi wake wa kujaribu bila tahadhari ulikuwa hatari na ulimgharimu maisha yake.
Back
Top Bottom