Baada ya sheria mpya kupitishwa iliyofuta FAO LA KUJITOA na kuja na mbadala wake wafanyakazi wengi hususani katika sekta binafsi walionja na wanaendelea kuonja joto la jiwe kutokana na kutoruhusiwa kuchukua MAFAO yao kwa mkupuo pale ajira zao zinapokoma ama kwa kumaliza mkataba au kwa kuachishwa kazi. Kile kilichohifadhiwa kama akiba ya mtu anapokwenda kukidai hakipati chote badala yake kuwa analipwa asilimia 33.3 kama sikosei ya mshahara wake wa awali.
Naamini kundi hili ni kubwa sana na kwa sababu sheria hii bado ipo na inaendelea kufanya kazi hata wale ambao bado ni watumishi wakati wa kumaliza mikataba yao au kuachishwa kazi utakapofika changamoto hiyo watakumbana nayo.
Hivyo kwa jinsi hali ilivyo akitokea mgombea urais yeyote akaishikia kibendera hoja hii ya FAO LA KUJITOA kwamba atalirudisha kama ilivyokuwa zamani atazoa kura nyingi sana na atapata kuungwa mkono na wananchi wengi.
Ewe mgombea urais kupitia chama chako wakati unatafuta kuungwa mkono na wananchi usisahau kutafuta kura zingine kwenye FAO LA KUJITOA na linadi kwa nguvu zote lipate kusikika masikioni na kunenwa vinywani mwa wananchi. Usidharau maana kura moja tu ina "impact" kubwa sana katika uchaguzi mkuu ujao.
CHAUMA, CUF, ACT- WAZALENDO, CCM na CHADEMA kazi kwenu. Sera zenu ziguse kila kundi fulani katika jamii. Kila mmoja ana hamu ya kusikia mgombea urais atakayekuja na majibu ya FAO LA KUJITOA
Niwatakie mpambano mwema katika kutafuta kuungwa mkono na wananchi katika harakati hizi za kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.