mkuu naona hii hoja imekugusa sana, kuongelea fao la kujitoa ni mawazo ya kienyeji sana,
Kwanza, kwanini mtu anadai fao lake? nikwa sababu kapoteza ajira "labor turnover" kinachopaswa kuangaliwa kwanini watu wapoteze ajira zao? Jambo la kwanza alilofanya mwalimu baada tu ya uhuru ni kufanya mtu kupoteza ajira kuwa jambo gumu. Na ndivyo inavyopaswa kuwa, kuwa mtu kupoteza ajira yake liwe jambo gumu sana.
Hawa wagombea wetu hakuna anayezungumzia job security, maelfu ya watu wamefutwa kazi kwa sababu mbalimbali, serikali ilipaswa iwajibike na hayo mambo ya hovyo kabisa. Lakini si Lissu wala jpm anaongelea hilo, tunatengeneza ajira na kupoteza ajira wakati huohuo work done equal to zero.