Fao la kuumia kazini malipo huwa yakoje unapopata ulemavu kabisa hasa wa kiungo chochote mwilini??

Fao la kuumia kazini malipo huwa yakoje unapopata ulemavu kabisa hasa wa kiungo chochote mwilini??

Chumvi yao

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2010
Posts
2,580
Reaction score
5,563
Niaje niaje jombaa..........natumaini mko poa mkiendelea na majukumu.........shida yangu ni kufahamishwa kama mtu alishawahi kupitia kitu kama hiki......nimepoteza kidole gumba cha mkono kwenye majukumu ya kazi ofisini........stahiki zangu ni zipi?? Naomba kufahamishwa tafadhali kwa mwenye uelewa ...Asante
 
Hapo watakao husika hapo na stahiki zako ni WCF (Workers Compensation Fund) ambapo kama kampuni yako ni mwanachama na wanalipa michango faili lako litapelekwa WCF hao ndio watakufidia. Ila kama kampuni yako si mwanachama wa WCF maana yake kampuni yako itawajibika moja kwa moja.
 
WCF na NSSF ndio watafanya malipo yote kama mwajiri wako alikuwa anapeleka makato yako kwao
 
Wasilisha madai/case kwa muajiri wako kwanza. Kwa taasisi zote zilizosajiliwa ni takwa la kisheria kuwa mwanachama wa WCF, na kama ni active member na anachangia mchakato wa kufile madai na kujaza form utaanzia hapo.
 
Back
Top Bottom