FAO yaishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha nchi soko la Kimataifa

Huu ni ukweli ambao sijui kwa nini wataalamu wetu hawaoni mpaka tuambiwe na FAO? The fact is that we spread yourself too narrowly. Tunalima mahindi, mpunga, ngano, viazi , maharagwe, kunde, ndizi, alizeti , michikichi, n.k, lakini siyo hata zao moja tunapeleka nje kama finished product. Ukienda Muheza utakuta malori mengi toka Kenya yanapakia machungwa, wanaenda kukamua juice halafu wanairudisha hapa kama finished product, hakuna mtu anayefikiria kuweka kiwanda Muheza au Tanga cha kukamua juice ya matunda.
 
Ardhi ya Tz Inakubali aina zote za mazao isipokuwa ya arabuni kama tende

Kikubwa fursa
 
Ni kweli, Ni wazo jema kabisa.

Tuwe na alama ya utambulisho kimataifa kupitia zao la aina moja ya kilimo.

Lakini haimaanishi kwamba tubweteke na tusitie nguvu katika kulima mazao mengine.
 
... mahindi yao kwa ajili ya kulishia nguruwe na cattle! Dah; this world is not fair.
Ndo ivo mkuu lakini ndo tayari maalufu kwa hilo na kuna wakati nilisikia kuwa hicho chakula cha wanyama kililetwa Africa kama msaada wakati wa njaa
 
Umenena vyema.
 
Nchi kama Tzn haiwezi kuwa na zao moja tuu,binafsi napendekeza tuwe na Mazao 5..

Happy tuwe na korosho,parachichi,mchele,chai na pareto.
 
Waende zao hapa!! Enzi za Mwalimu Nyerere tulikuwa na Pamba,Kahawa,Mkonge ,Chai na Muhogo kama Exports.Na tulikuwa Vizuri sana .Sasa hivi Wanaotuangusha ni Wanasiasa .Kama wakiwa makini Tanzania tutarudi no 1 kwenye export za mazao ya Kilimo
Swma hivi tuyape kipaombele Mazao machache sio tunaenda jumla jumla tuu..

Tuchague Mazao maalum for exports kama 5 na Mazao ya food security for domestic and exports when needed.
 
Wazo zuri sana
Akitoa mzungu ndio linakuwa wazo zuri ila tukisema wananzengo haina maana?

Mawazo yamezungumzwa Sana hata saizi ukienda story of change kuna mawazo mazuri mengi tuu ila mnasubilia aje mzungu ndio aseme .
 
Akitoa mzungu ndio linakuwa wazo zuri ila tukisema wananzengo haina maana?

Mawazo yamezungumzwa Sana hata saizi ukienda story of change kuna mawazo mazuri mengi tuu ila mnasubilia aje mzungu ndio aseme .
ndio mfumo tulio rithiswa na wakoloni shekh ndio maana hadi leo ni zaidi ya miaka 70 bado tunaitumia Katiba yao
 
Ndo ivo mkuu lakini ndo tayari maalufu kwa hilo na kuna wakati nilisikia kuwa hicho chakula cha wanyama kililetwa Africa kama msaada wakati wa njaa
Mahindi ya Yanga wazee wanasimulia.
 
Wamepotea, hatutafuata hivyo kamwe.

Mazao ya biashara nje yanafahamika toka enzi hizo na yataendelea kuwa hivyo, hatutapiga mark time.
Mnapenda kukariri na upeo ni mdogo na elimu vilevile.
 
Wazo la Kijasusi. Hatulitaki. Tumekataa. Shenzi kabisa. Hivi wanatuonaje hao?
 
Kilimo Cha karanga KONGWA
Ha ha ha mzee mwenzangu mitaala ya elimu tuliyokuwa nayo ni ya kijinga sana. Eti rais wa kwanza wa Mali aliitwa nani? Wakati wenzetu huko walikuwa wanasoma mambo ya teknolojia na kadhalika, sisi tumebaki kuwasifu kina Kwame Nkurumah.
 
My take; Pendekeza zao, binafsi Napendekeza Korosho
Una sababu zipi, kwa nini isiwe soya, ukiniuliza ntakupa sababu kikamilifu.

Hata hivyo sikubaliani na wazo hilo la zao moja. Nchi yetu ina maeneo yenye kubeba aina tofauti za mazao. Kupeleka korosho Kilimanjaro haitasaidia sana wananchi wa huko. Brazil ina Kahawa na Soya na mifugo, kama kuku n.k. Kwani Kenya kuwa na zao la chai ni kipi kimeongezeka kwao? Mbona wanahangaika na Avocado, Maua, mbogamboga, n.k.

Zao moja likibuma kutokana na sababu mbalimbali, hali ya hewa, au hata kushuka kwa bei duniani, ndiyo mmekwisha kazi msimu huo!

Hilo ni pendekezo la hovyo. Huyo mtu kakosa jambo la muhimu la kujadili na waziri wetu, akaona heri apoteze muda akipiga soga.

Lakini sikusoma sababu yake kushauri hivyo, Bado sidhani kuwa ni ushauri wa kuwekwa maanani.

Pendekezo la maana sana angesema MIKOA iwe na zao moja la nguvu sana. Kwa mfano, Kigoma yote ile ingeenezwa na michikichi sehemu zote za mkoa.
Kagera ikajichimbia kwenye NDIZI na Kahawa

SIMIYU PAMBA

SIngida na Dodoma usiwaambie chochote zaidi ya ALIZETI, n.k., n.k..
 
Wamesema zao la kipaumbele!
EeenHeeee!

Kweli umekengeuka kwenye hili. Akili imegota kabisa!
Heri ubaki kwenye siasa za CCM na vimistari vyako viwili viwili.

"Kipaumbele" maana yake nini,...kama michikichi inastawi vyema Kigoma, tuamue hilo zao ndio liwe wakilishi wa nchi nzima, kwa kulipa "kipaumbele", kama ndilo zao tunaloweza kuchagua kuwa litutambulishe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…