JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 706
- 1,230
Kuna filamu ya Kikorea ya mwaka 2023, iitwayo Unlocked, inayotoa funzo kubwa kuhusu usalama wa kidijitali na hatari za uhalifu wa mtandaoni.
Filamu inamuhusu Nami, aliyempelekea fundi simu yake kwa matengenezo. Kama wafanyavyo mafundi wengi, aliichukua simu na Kwenda nayo nyuma, ambako Wateja hawaruhusiwi kufika. Nami, akiwa na imani kwamba fundi ni mkweli, alimkabidhi simu yake bila wasiwasi. Lakini fundi huyo alitumia nafasi hiyo vibaya — akaweka kamera ndogo ndani simu, kisha akaifunga vizuri kama haijaguswa.
Awali, alimwomba Nami password kwa kisingizio cha kujaribu simu baada ya matengenezo, na Nami alimpa. Kwa kutumia password hiyo, fundi aliunganisha simu kwenye kompyuta, akaweka faili la siri, na baadaye aka-clone simu nzima — akatengeneza nakala kamili ya simu ya Nami. Kuanzia hapo, kila kitu ambacho Nami angefanya kwenye simu yake, fundi angeweza kukiona kupitia simu nyingine aliyokuwa nayo.
Nami hakujua kuwa faragha yake ilikuwa imevunjwa kabisa. Fundi alianza kuona kila kitu: picha, ujumbe, simu, hata kuwasha kamera bila ruhusa. Kadiri siku zilivyoendelea, alianza kumfuatilia — akajua anapenda vinywaji gani, michezo (games) gani, muda wake wa kulala na kuamka, hadi ratiba yake ya kwenda kazini.
Fundi aligundua kuwa Nami alikuwa karibu na bosi wake na anatarajia kupandishwa cheo. Akaanza kuchunguza undani wa maisha yake — akajua watu wa karibu. Hatimaye akaanza kumfuatilia kimwili (Physically). Alienda kwenye mgahawa ambako Nami alikuwa akifanya kazi ya ziada, akaagiza vinywaji anachopenda Nami, jambo lililomvutia Nami kwani walionekana kufanana kwa mambo mengi.
Siku moja usiku, rafiki yake Nami alifika nyumbani akisema amepokea mwaliko kutoka kwa Nami. Nami alishangaa, kwani hakuwahi kutuma ujumbe huo, lakini hawakuwaza sana, walikaa — bila kujua fundi alikuwa akisikia kila mazungumzo kupitia simu.
Asubuhi iliyofuata, Nami alipata zaidi ya 80 missed calls kutoka kwa bosi wake. Aliona akaunti zake za mitandao ya kijamii zikilipuka kwa arifa na matusi. Ndani ya kundi sogozi la ofisi, kila mtu alikuwa akimkashfu. Alipochunguza, aligundua machapisho yaliyokuwa yakifichua siri za bosi wake na tuhuma dhidi ya wenzake, yote yakitoka kwenye akaunti zake mwenyewe.
Akiwa amechanganyikiwa, alifika kazini — lakini bosi wake, akiwa amejaa hasira, alimfukuza.
FUNZO KUTOKA KWENYE FILAMU HII
Yaliyotokea kwenye filamu hii kuhusu fundi yanaakisi hali halisi katika jamii zetu — mambo tunayoyaona kuwa ya kawaida lakini yanaweza kuleta madhara makubwa. Ni muhimu kuchukua tahadhari zifuatazo:
1. Usiamini kirahisi kuhusu vifaa vyako vya kidijitali: Kama ilivyomtokea Nami, wengi hupeleka simu kwa mafundi bila kujua kama wanaweza kutumia vibaya taarifa zetu. Kumbuka, simu ni kifaa binafsi chenye picha, ujumbe, na nywila. Hakikisha unaipeleka kwa fundi unayeamini au kituo rasmi cha huduma.
2. Linda nywila zako (passwords): Nami alimpa fundi nywila yake kwa urahisi, jambo lililomgharimu faragha yake. Nywila ni kama ufunguo wa maisha yako ya kidijitali — usimpe mtu yeyote bila sababu ya msingi. Ikiwa utalazimika kufanya hivyo, badilisha nywila mara baada ya huduma.
3. Teknolojia inaweza kutumika vibaya: Filamu inaonesha jinsi vifaa vidogo kama kamera au teknolojia ya cloning vinavyoweza kutumika kuvunja faragha. Hii inatukumbusha kuwa si lazima uhalifu wa mtandaoni ufanywe na “hackers” pekee — hata watu wa karibu wanaweza kutumia teknolojia vibaya.
4. Tambua alama ndogo za hatari: Nami hakugundua mapema kuwa fundi alikuwa anamfuatilia kwa sababu kila kitu kilionekana cha kawaida. Dalili kama simu kuwa na matatizo yasiyoelezeka, kamera kuwashwa bila ruhusa, au matumizi ya data yasiyo ya kawaida zinaweza kuwa ishara za hatari, utumaji wa ujumbe ambao haujauidhinisha.
5. Faragha ni sehemu ya utu wetu: Wengi hatutambui kuwa kulinda taarifa binafsi ni haki ya msingi. Filamu hii inatukumbusha kuwa uvunjaji wa faragha unaweza kuathiri maisha ya mtu — kihisia, kijamii, na hata kiuchumi.
Kwa ujumla, Unlocked inatufundisha kuwa katika dunia ya kidijitali, kulinda usalama wa taarifa binafsi si hiari — ni wajibu wa kila mmoja wetu kila siku.