Farhan wa Clouds FM: Wanaomtuhumu Heche, zikija hoja za 'No Reforms, No Election', Free Lissu huwaoni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mtangazaji wa Clouds FM, Farhan, ameeleza mtazamo wake kuhusu wimbi la tuhuma zinazomkabili Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, akisema kuwa kuna aina ya watu na hata baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao wamekuwa mstari wa mbele ku-comment kwa kudaiwa kula fedha za chama.

Hata hivyo, Farhan amebainisha jambo la kushangaza kuwa, watu hao hao waliopo mstari wa mbele kumtuhumu Heche sasa hivi, huwa hawaonekani kabisa pindi chama kinapokuwa na hoja na ajenda nzito za kitaifa kama vile msimamo wa "No Reforms, No Election" au kampeni za kumtetea Tundu Lissu.

Your browser is not able to display this video.
 
Kabla hauja comment sikiliza kwanza
 
Hoja ni utafunwaji wa fedha za chama unaofanywa na Heche. Farhan Anataka kuhamisha mjadala.
 
no elections no reform was useless and completely nonsense narrative ndio maana chadema wengi waliipuuza 🐒
 
Hata kama Heche kazipiga kweli mbona Mwamba alipozipiga hatukusikia hizi kelele zote?

CDM ishapata hadi hati za ukaguzi zenye mashaka kutoka kwa CAG na hatukuwasikia hawa watu!

Sasa hivi ndiyo wana uchungu sana na pesa za chama?

Huu ni mradi tu unasukwa na muda si mrefu lengo lake litakuwa wazi.
 
Mwamba mbona umeshusha essay bila kusikiliza na kusoma mada hiki ndicho ndugu yetu Pascal Mayalla anakizungumzia ndio maana hadhi la hili jukwaa linazidi kushuka watu wanatoa michango kwa kuendeshwa na mihemko na hisia badala ya nguvu ya hoja.
 

Ni maajabu Kwa kweli.
 
Yuko sahihi KABISA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…