Farid Musa Ulaya ndio basi tena?

Kama mchezaji unataka maendeleo yako ya we kimataifa usimshauri kijana aende Simba au Yanga hawana maono ya baadae ya mchezaji!Kwa mfano samata alivyokuwa To mazembe angeamua kurudi nyumbani nafikiri saizi angekuwa anacheza ndondo pale chanika
 
Kama mchezaji unataka maendeleo yako ya we kimataifa usimshauri kijana aende Simba au Yanga hawana maono ya baadae ya mchezaji!Kwa mfano samata alivyokuwa To mazembe angeamua kurudi nyumbani nafikiri saizi angekuwa anacheza ndondo pale chanika
Ila huyo Samata ndiye aliyemshauri Farid aende Yanga kwa lengo kwamba angepafomu vizuri ingekuwa rahisi kurudi ulaya. Sasa kijana mwenyewe kila akipewa nafasi anashindwa kuichukua
 
Kama mchezaji unataka maendeleo yako ya we kimataifa usimshauri kijana aende Simba au Yanga hawana maono ya baadae ya mchezaji!Kwa mfano samata alivyokuwa To mazembe angeamua kurudi nyumbani nafikiri saizi angekuwa anacheza ndondo pale chanika
Uzembe wake mwenyewe halafu analaumiwa Simba na Yanga mbona wachezaji wengi tu wamepita hivyo vilabu na kufika mbali akiwemo Simon Msuva, Dikson Kibabage, Samata, Sunday Manara, Boban, Shaban Nonda na wengineo.?
 
Ucheze Yanga halafu uende Ulaya? Mtanzania? Haijawahi tokea
Mtanzania wa Kwanza kucheza Ulaya ni kijana kutoka Yanga Sunday Manara aliyekwenda kukipiga Uholanzi, kipindi icho Uholanzi kulikua na Magwiji wa soka Duniani, Mwenzake Maulid Dilunga kutoka Yanga alikua Mtanzania aliyechaguliwa kikosi Bora Cha mastaa wa Afrka kilicho kwenda Mexico achana na wakina Athmani Abdala China aliyekwenda England au Shaaabani Nonda mkongoman aliye anzia Yanga mbaka kucheza fainali ya Mabingwa ulaya akiwa na Monaco.
Washawahi kuja Mabingwa wa zamani wa ulaya Astonvilla ya England wakatoka sare ya 1-1 na Yanga pale shamba la Bibi, Baada ya Astonvilla kusawazisha bao. Yanga sio kitu cha masihara, Kama wakijipanga huwa awazuiliki.
 
Kuna haja kubwa sana kwa wale wenye uwezo wa kuandika makala/vitabu/hadithi watusaidie watanzania kuandika historia ya jinsi wachezaji wa Tanzania walivyoenda kucheza Ulaya walitumia njia gani na walipata misukosuko gani mpaka mafanikio yao. Na hapa wanaweza kuanza na Mbwana Samata na Sunday Manara "Computer". Na si vibaya pia wakaandika kuhusu wale walioshindwa kufanikiwa kucheza Ulaya ili kujua walikumbwa na changamoto gani. Pili waandae makala za namna wachezaji wa West Afrika wanavyoenda Ulaya. Maandishi yote hayo yakikusanywa halafu yakawa yanafundishwa kwa vijana wetu waliopo kwenye "Academy" zetu na pia yakasomwa na vijana waliopo VPL na ligi daraja la kwanza naamini baada ya miaka michache ijayo tutakuwa na watanzania wengi wanaocheza Ulaya. Pamoja na hayo wafundishwe saikolojia na namna ya kupambana wakiwa nje ya nchi sehemu ambayo hakuna baba wala mama achilia mbali ndugu wa karibu wa kukusaidia. Maandishi hayo yanaweza kutumiwa kama mtaala usio rasmi kwa ajili ya vijana wanaotaka kwenda kucheza mpira wa kulipwa nje.

Naamini kabisa iwapo Farid angekomaa Hispania angetoboa na iwapo angefeli kabisa basi angeangukia kwenye ligi hata ya Uturuki huko lakini sio kurudi bongo. Na Farid ni muendelezo ule ule wa wachezaji wa kitanzania wenye vipaji vikubwa tena vya asili lakini wanakosa uvumilivu na moyo wa kupambana Ulaya wanaamua kurudi bongo; kama ilivyokuwa kwa kaka zake Mrisho Ngassa, Haruna Moshi "Boban", Jerry Tegete, Shomari Kapombe na kaka yake mwingine mzembe kabisa Ajib aliyekataa kwenda TP Mazembe akabaki Simba ambayo haimtaki sasa. Na kiwango cha Farid sasa hivi kimeshuka sana kiasi hata Yanga leo hii wakisema wanamuacha kwenye usajili Simba na Azam hazitamsajili hata bure kabisa.
 
Kwani kisa cha kutoka kwa FARID hispania kilikua kipi?
 
Watanzania wa kuandika makala ya kiuchunguzi kama hii ni wachache sana.

Ila Mwananchi wana waandishi wa habari angalau labda wanaweza kufanya hiyo kazi!
 
Watanzania wa kuandika makala ya kiuchunguzi kama hii ni wachache sana.

Ila Mwananchi wana waandishi wa habari angalau labda wanaweza kufanya hiyo kazi!
Tena ingewezekana serikali ingefadhili hili zoezi kwa sababu michezo hususani mpira wa miguu ni fursa na chanzo kikubwa cha ajira duniani
 
Kwani kisa cha kutoka kwa FARID hispania kilikua kipi?
Ni uzembe, homesickness, kukata tamaa na mbaya zaidi kufikiri kuwa kucheza ligi kubwa duniani ni rahisi . Bila kujua kuwa kwa mchezaji anayetoka kwenye nchi zilizo na viwango vya chini kwenye "rank" za FIFA anahitajika kuwa mvumilivu na "sacrifice" ya hali ya juu ili kufikia viwango vya kucheza ligi kubwa.
 
Farid alienda nchi ngumu sana.
spain siyo nchi sahihi kwa wachezaji wa tanzania kwenda kuanzia kucheza.

Ni nchi ambayo bado vilab vyake havija appreciate uwezo wa wachezaji weusi kutoka africa wanaoenda huko moja kwa moja.

Labda tu youth career ya farid ingeanzia palepale.

Pili by statistics wachezaji weus spain ni wachache ukilinganisha na belgium, norway, france nk

Sijui umri wake lakini nchi nzuri ni swis, austria au finland.

Farid yeye alitua CD Tenerife..kwa free transfer akitokea azam
pale aliwakuta ma-striker wanne wazungu wazoef
akiwamo SUS0.

Huyu bwana SUSO aliwahi kucheza liverpool baadaye akauzwa.
farid alimkuta pale kaja kwa mkopo toka club fulan jina limenitoka.

Tenerife ilikuwa timu kubwa kwake.ipo daraja la pili.
 
Tatizo la wachezaji wengi wa kitanzania wanatamani kuwa kama Samata lakini hawachukui muda kujifunza kwa Samata kujua alipita njia gani kufika hapo alipo. Mfano mdogo tu kocha Phiri kutoka Zambia aliyemfundisha Samata anasema kuwa Samata alikuwa anafika saa kumi na mbili asubuhi uwanja wa taifa kutoka Mbagala na alikuwa anafanya mazoezi ya peke yake kabla ya mazoezi ya timu nzima ya Simba yaliyokuwa yanaanza saa mbili asubuhi. Moja kwa moja unaona mbali ya kipaji cha mchezaji binafsi kunahitajika kujituma, nidhamu na uvumilivu wa hali ya juu sana. Samata kaanzia safari yake hapa Tanzania kwenda kucheza ligi kubwa Ulaya na kafanikiwa kwa sababu alikuwa kajipanga vizuri lakini Farid karahisishiwa safari kutoka tu Azam fasta kapelekwa Hispania japo daraja la chini lakini kachemsha karudi bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…