Farid Musa Ulaya ndio basi tena?

Farid Musa Ulaya ndio basi tena?

Kuna haja kubwa sana kwa wale wenye uwezo wa kuandika makala/vitabu/hadithi watusaidie watanzania kuandika historia ya jinsi wachezaji wa Tanzania walivyoenda kucheza Ulaya walitumia njia gani na walipata misukosuko gani mpaka mafanikio yao. Na hapa wanaweza kuanza na Mbwana Samata na Sunday Manara "Computer". Na si vibaya pia wakaandika kuhusu wale walioshindwa kufanikiwa kucheza Ulaya ili kujua walikumbwa na changamoto gani. Pili waandae makala za namna wachezaji wa West Afrika wanavyoenda Ulaya. Maandishi yote hayo yakikusanywa halafu yakawa yanafundishwa kwa vijana wetu waliopo kwenye "Academy" zetu na pia yakasomwa na vijana waliopo VPL na ligi daraja la kwanza naamini baada ya miaka michache ijayo tutakuwa na watanzania wengi wanaocheza Ulaya. Pamoja na hayo wafundishwe saikolojia na namna ya kupambana wakiwa nje ya nchi sehemu ambayo hakuna baba wala mama achilia mbali ndugu wa karibu wa kukusaidia. Maandishi hayo yanaweza kutumiwa kama mtaala usio rasmi kwa ajili ya vijana wanaotaka kwenda kucheza mpira wa kulipwa nje.

Naamini kabisa iwapo Farid angekomaa Hispania angetoboa na iwapo angefeli kabisa basi angeangukia kwenye ligi hata ya Uturuki huko lakini sio kurudi bongo. Na Farid ni muendelezo ule ule wa wachezaji wa kitanzania wenye vipaji vikubwa tena vya asili lakini wanakosa uvumilivu na moyo wa kupambana Ulaya wanaamua kurudi bongo; kama ilivyokuwa kwa kaka zake Mrisho Ngassa, Haruna Moshi "Boban", Jerry Tegete, Shomari Kapombe na kaka yake mwingine mzembe kabisa Ajib aliyekataa kwenda TP Mazembe akabaki Simba ambayo haimtaki sasa. Na kiwango cha Farid sasa hivi kimeshuka sana kiasi hata Yanga leo hii wakisema wanamuacha kwenye usajili Simba na Azam hazitamsajili hata bure kabisa.

Zipo Sana
Ungesoma ya Boban ungelia
 
Nafikiri badala ya kubaki makabatini wajitokeze watu wazikusanye watengeneze kama kitabu hivi wapewe wakina Ivo Mapunda wenye hizi "Academy" ziwasaidie watoto wa kitanzania kwa siku zijazo ili wasije kuwa kama wakina "Boban"
Vitabu hii nchi havisomwi
Watengeneze makala "documentaries" au wampe diamond atengenezee wimbo
 
Back
Top Bottom