Faridi Mussa MAMBO SAFI, Kutua Tenerrife

Faridi Mussa MAMBO SAFI, Kutua Tenerrife

PROSPER 05

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
226
Reaction score
217
Winga wa Azam Farid Mussa muda wowote anaweza kuondoka nchini kwenda nchini Hispania kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya CD Tenerrife baada ya kupata kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini Hispania.
Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC, Nassor Idrissa ameiambia Goal (mtandao wa goal (2/12/2016), klabu hiyo wametuma kibali hicho na tayari wamekabidhi mchezaji mwenyewe ili aweze kufanya maandalizi ya safari.

“Kama uongozi tunafurahi kwa jambo hili kukamilika kwasababu kulikuwa na maneno mengi yanasemwa mtaani kwamba sisi Azam tunambania Farid, lakini leo ukweli imejulikana,”amesema Idrissa.

Mwenyekiti huyo amesema kwa muda mrefu mchezaji huyo alikuwa kambini kwao akipata huduma zote lakini walishindwa kumtumia kwasababu walishatuma ITC yake kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania.

Kwaupande wake Farid amesema anajisikia furaha kupata kibali hicho na anakwenda Tenerrife, lengo likiwa moja tu kufanya vizuri na kuifika mbali kwenye maisha yake ya soka.

Mchezaji huyo amesema kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza mashindano yoyote kumempa hasira hivyo atahakikisha anakwenda kujituma ili aweze kutimiza ndoto nyingi alizojiwekea ikiwemo kucheza klabu kubwa za nchi hiyo.

“Nataka kucheza Barcelona au Real Madrid na hiyo ndiyo nafasi pekee ambayo kama nikiitumia vizuri naweza kutimiza kile nilicho kikusudia.

Tenerrife Ilivutiwa na kiwango cha Farid, baada ya mchezaji huyo kwenda kufanya majaribio Aprili mwaka huu na kufanya vizuri kiasi cha benchi la ufundi la timu hiyo kumuhitaji moja kwa moja.

My Take: Mashabiki Wazalendo tumefurahishwa na mpango huo na tuna matumaini Farid atawawakilisha vyema huko anapokwenda na kuitangaza Tanzania kutokana na kiwango alichokuwa nacho. Pia Nashauri Timu yangu ya AZAM wamsaidie Huyu Dogo Kama ni Maslahi Makubwa Watayapata Baadae.
faridi Mussa.jpg
 
Ni vzr kuwa na expectation kubwa kama za kwenda Barca na Real
 
Mpira wa bongo uko Kama bongo movies
 
Wazalendo watu wa mpira tunapata faraja kupata habari kama hizi, potelea mbali hata kama ni moja kwa mwaka.
 
Sitoamini hadi nione kapanda ndege
Kilichokua Akizungumzwi ni MASLAHI, Teneriffe walitaka Kumnunua Lakini AZAM hawakuafiki Dau hivyo wakaona Bora wamtoe kwa MKOPO. Wameshakubaliana Atoke kwa Mkopo. Hivyo Faridi Bado ni Mchezaji wa AZAM...
 
Back
Top Bottom