Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Jumla ya wanafunzi 134 wavulana 72 na wasichana 62 wamehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari katoro day huku wakitakiwa kusimamia ndoto zao, ili kukabiliana na changamoto za maisha, jamii, familia na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi [UVCCM] Mkoa wa Kagera Comred Faris Buruhani Desemba 03, 2024 wakati akishiriki katika mahafali ya 14 shuleni hapo.
Akizungumza na wanafunzi hao Faris amewasihi kuhakikisha wanakabiliana na changamoto na vikwazo vitakavyowakabili mtaani ili kukidhi kiu ya wazazi wao wanaowategemea.
Aidha, amewasisitiza kuhakikisha wanasimamia ndoto zao na wala wasiogope kujaribu na kujitolea kwa kuwa elimu ya darasani ni msingi wa kuanza safari na kujua kufanikisha lakini safari ya maisha inahitaji kujituma ujasiri na ushirikiano.
Kwa upande wake mkuu wa Shule hiyo amesema Shule ya sekondari Katoro day ina mpango wa kuendelea kuboresha taaluma shuleni hapo Kwa kuwa ndio lengo kuu la Shule ambayo imefanikiwa kuongeza idadi ya Wanafunzi wanaomaliza na wanaojiunga na kidato cha kwanza.
ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA