carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Buruhani, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza katika kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia wizara, halmashauri na taasisi mbalimbali za kifedha.
Akizungumza Oktoba 31, 2026, wakati wa mapokezi yake mkoani Kagera, Buruhani alisema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana na kuweka utaratibu unaotaka asilimia 30 ya manunuzi ya umma kuelekezwa kwa makundi maalumu, yakiwemo vijana, kwa mujibu wa sheria na taratibu husika.
Aidha, Buruhani ametoa onyo kwa viongozi wa UVCCM katika ngazi za mikoa, wilaya na kata, akisema wanapaswa kuweka mbele maslahi ya vijana na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.
Alisema mwaka 2027 chama kinatarajiwa kuingia katika uchaguzi wa ndani, hivyo viongozi wanaotaka kuendelea au kupata nafasi za uongozi wanapaswa kuonyesha kwa vitendo namna wanavyopigania maslahi ya vijana.
“Yeyote atakayekaa kwenye uongozi wa mkoa au wilaya akashindwa kutatua shida za vijana, huyo tunamtafutia mlango wa kutoka,” alisema Buruhani.
Ameongeza kuwa dhamira yake ni kuhakikisha viongozi wa UVCCM wanawajibika na kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya vijana, akisisitiza kuwa uongozi unapaswa kupimwa kwa uwezo wa kutatua changamoto za wananchi wanaowawakilisha.