Sio kwamba aliichukia Kenya, maanake Kenya ndio ilifanikisha azimio lake na mipango yote hadi akawa rais. Hapo awali, enzi za rais Mwai Kibaki, Farmajoo alikuwa anaishi Kenya na kutawala nchi yake kutoka jijini Nairobi.
Bifu zake na Kenya zilianza alipostukia mipango ya Kenya kule Jubaland. Eneo ambalo limepakana na Kenya na ambalo linataka kujitenga rasmi na nchi ya Somalia. Rais Uhuru alilazimisha kuwe na uchaguzi Jubaland, kabla ya muda. Kisa Kenya ilitaka Rais Sheikh Ahmed Madoobe aendelee kuitawala Jubaland. Uchaguzi ulifanywa Kismayu, licha ya pingamizi za Farmajoo na serikali kuu ya Mogadishu.
Sheikh Madobe akashinda kwa kishindo, jambo ambalo Farmajoo hakulitarajia. Ikawa wazi kwamba Nairobi ina ushawishi mkubwa Kismayo, zaidi ya serikali kuu kule Mogadishu. Rais Sheikh Madobe akisaidiwa na Kenya, kihali na kimali, amekuwa tishio kubwa sana kwa Mogadishu. Kikosi chake cha Ras Kamboni Brigade kimeimarika sana. Baada ya kufanyiwa mafunzo na kufanya kazi na KDF kwa muda mrefu, wakipagana kwa pamoja dhidi ya magaidi wa alshabaab.
Zaidi ya hayo, silaha na vifaa vya kivita vinafika Kismayu, Jubaland moja moja kwa moja kutoka Nairobi, chini ya ufadhili wa serikali ya Kenya. Baada ya rais Uhuru kuwakubalia wapinzani wote wa Farmajoo kufanya vikao vyao vya kampeni kutoka Nairobi. Jamaa akaanza kupanick na kujaribu kuleta chuki kati ya Kenya na Somalia, ili apate kura za huruma. Ila hamna namna sasa, itabidi afunganye virago vyake roho safi na arudi kwao US.