Faru 9 weusi waingizwa nchini kutoka Afrika Kusini ikiwa ni jitihada ya kurejesha jamii hiyo iliyo hatarini kutoweka

Faru 9 weusi waingizwa nchini kutoka Afrika Kusini ikiwa ni jitihada ya kurejesha jamii hiyo iliyo hatarini kutoweka

Joined
Oct 12, 2019
Posts
28
Reaction score
15
Faru 9 weusi wameingizwa #Tanzania kutoka Afrika Kusini ikiwa ni jitihada za kurejesha jamii hiyo ya faru iliyopo hatarini kutoweka, kutokana na ujangili uliofanyika kipindi cha nyuma.

Shirika la CITES, linalohusika na wanyama waliopo hatarini kutoweka linakadiria hadi 2015 kulikuwa na faru wa jamii hiyo 133 nchini Tanzania.

Faru hao wameletwa na Grumeti Fund, wanaohusika na utunzaji wa wanyama pori.
 
Hongera Magufuli kwa kujali raslimali zetu

Viongozi waliopita walikuwa wanauza raslimali kwa Mabeberu
 
Habari njema hizi. Hawa Grumeti pia wana hotel huko mbugani.
 
Nyalandu yupo wap? Katutia hasara Sana,
Acha unaaa!! Waliokutia hasara hujui wapo wapi kwa sasa? Kwani ndiye alikuwa Rais? Alikuwa waziri kwa muda gani? Ile meli iliyokamatwa na meno ya tembo ilikuwa yake?wakati hayo yanafanyika bunge lilikuwa wapi, na nyie wenye uchungu na nchisi ndio mlikuwa wengi bungeni ni hatua gani mlichukua kulizuia?!! Acheni unafiki. Kote ni uozo na chanzo ni nyie leo mnajifanya eti mnashangaa na kutaka sifa tena, wakati ndio mliotufikisha hapa!!!
 
Hongera Magufuli kwa kujali raslimali zetu

Viongozi waliopita walikuwa wanauza raslimali kwa Mabeberu
Mkuu si kwa commet hiyo. Mara nyingi tunanukuu mambo ya maana sio ya kijinga, viongozi kama wanadamu wanakosea pia.Mtazamo na kauli hasi ya mkuu dhidi ya Watangulizi tumsamehe ulimi uliteleza.
 
Back
Top Bottom