Mwanaone, maelezo yako yanadokeza wewe nimmoja wa wadau watakaonufaika na hiyo training ya Fast Track ambayo kwa kweli si lolote ni uchakachuaji tu. Unasema Diploma ya UUguzi miaka 4 ni upuuzi? Unataka kutushawishi kwamba wahitimu wa miaka 2 unayotaka watakuwa competent sawa na wa miaka 4? Kwa msingi upi wa elimu kama sote tunafahamu jinsi viwango vya elimu vilivyoshuka nchini? zaidi ya nusu ya wahitimu wa vidato vya nne na sita na hata baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu siku hizi hawawezi kujieleza kwa lugha ya kiingereza kwa ufasaha, je, hujui kwamba hiyo ndiyo lugha rasmi kwa kufundishia Uuguzi na Uganga?
Uuguzi na uganga una terminologies ngumu kufahamika hata kwa wanaoifahamu vema lugha hiyo na zamani wanafunzi waliandaliwa kwa mwaka mzima wakifundishwa pamoja na mengineyo lugha ambayo baadae itakuwa lugha yao rasmi ya kikazi, sasa kwa hii lipualipua ya kina Kikwete unadhani wataupata kweli muda huo? Kisha kulikuwa na mwaka mzima wa Ukunga (Midwifery) ambapo wanafunzi walijifunza kwa vitendo wakikaguliwa kwa karibu kabisa na wakuu wa idara husika na waalimu wao; jambo lililosababisha wauguzi wetu kuonekana competent hata nje ya mipaka yetu, leo hii taifa letu linajivunia wauguzi tele walioajiriwa na kuaminika Afrika Kusini, Botswana, Swaziland na mpaka Canada, Uingereza na Marekani, unadhani hali itakuwa hivyo baada ya zoezi hili? Mnalinganisha eti na nchi zilizoendelea, sisi tumeendelea? tuna zana za kufundishia zilizo sawa na wanazotumia wanafunzi wa Uingereza, Uholanzi n.k.? na tumeangalia vema background ya wanafunzi watarajiwa wetu?
Vyovyote ilivyo huu ni uchakachuaji na inabidi ulaaniwe kwa nguvu zote. Wamechakachua shule za msingi tukanyamaza, shule za sekondari tumenyamaza, na sasa kwenye sekta nyeti ya afya tunyamaze? Hapana. Nasikia sasa wanachakachua hata kwenye majeshi maana nasikia kuna maofisa wanaoitwa Voda Fasta yaani watoto wa vigogo wanaosukumwa tu mradi wahitimu mafunzo! Nauliza tunakwenda wapi?
Mungu ibariki Tanzania.