Fastjet ni kero tupu!

Fastjet ni kero tupu!

mojaone

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
135
Reaction score
30
Habari zenu wanajamvi,

Kuna baadhi ya mambo yananichanganya kuhusu hawa fastJet,

1.Bei zao wanazotutangazia hazina ukweli wowote na hazikaribiani na ukweli,
Mfano leo kwenye website yako wamatutangazia ndege yao ya kwanza kutoka Dar kwenda KIA ni tsh32,000 ,nimepiga simu wanasema ni Tsh107000=.

2.Ukichelewa hata dakika moja baada ya reporting time hawakujui,kwani wameshachukua chao,wanakunyima safari.Hii imemtokea jamaa yangu mmoja leo jioni,walikuwa zaidi ya abiria 8 lakini hawakuwasikiliza zaidi ya kuwapa majibu ya kukatisha tamaa na kejeli,

3.majibu yao kwa ujumla wanaonekana kama abiria wanaopanda hiyo ndege wanapanda bure,au ni kama msaada flani,hawamthamini abiria kabisa,

4.Watanzania wenzangu tunaofanya hapo fastjet na wateja ebu jaribuni kuipa thamani pesa yetu ilingane na huduma tunayopewa na tunayotoa kwa wateja,hatuhitaji msaada wenu,

Mwenye kero kama zangu tiririka hapa
 
Unalipa 32000 au hata 100,000,kwenda kurudi kj na unachelewa???nyie ndio wapuuzi wote 8,mshafanya hilo daladala.basi la mkoa lenyewe halisubiri abiria itakua ndege.nawapa sifa hao staff maana wangewaendekeza nyie itakuwa taabu mtataka hata kutumiwa gari nyumbani kuwachukua na buku 30 zenu nyambaf.
 
Wabongo ukiwachekea hawakawii kumwambia rubani asimame chalinze wanunue nazi za kwenda nazo moshi.

Tena watataka badala ya kutua kia, ndege iwe inashusha na kupakia njiapanda ya imo, kiboruroni nk.
 
dah hii kali hata traine ya mwakiembe haiendi hivyo jamani,wabogo bwana! Nimecheka hadi basi!
Wabongo ukiwachekea hawakawii kumwambia rubani asimame chalinze wanunue nazi za kwenda nazo moshi.

Tena watataka badala ya kutua kia, ndege iwe inashusha na kupakia njiapanda ya imo, kiboruroni nk.
 
Waache hizo,, watu tushachelewa qatar, ndege ya saa 7 tumefika airport saa 6 tulikuta wameshafunga sehem zao za check in na computer zimeshazimwa lakini walikuja wakawasha computer na waka print sticker zao za mabeg tukafanyiwa check in fasta as emergence na tukaingia as kama tulikuwa tunasubiriwa sisi as tulivyoingia tu ndo ndege ikafungwa na kuanza kuondoka..

Sembuse hao wa dakika 1,,, sizani kama kuna ndege inamtosa abiria kwa dakika 1... Na hata KLM nilishachelewa ORD na bado hawakufunga fasta tukafanyiwa check in na tukaingia...

Kila abiria wakimtosa kuchelewa si itakuwa balaa kwenye connections mfano you have almost 3 connections to final destinations so ukiikosa ndege ya kwanza transit zote zinaharibika as sio kila sehemu kuna daily flights.. Mfano ukiachwa na turkish may be in chicago inabid usubiri 2 days kupata connection ya turkish from instanbul to dar si balaa hilo na kama imejaa si wiki nzima inakula kwako upo airport tu...

Hao fast jet hata kama ni ku keep time wamezidi maana hata international airline hazipo systematic kiasi hicho
 
Wabongo ukiwachekea hawakawii kumwambia rubani asimame chalinze wanunue nazi za kwenda nazo moshi.

Tena watataka badala ya kutua kia, ndege iwe inashusha na kupakia njiapanda ya imo, kiboruroni nk.

Mkuu hiyo mbona ishatokea KIA watu tulikaa kimya tuu yaani sasa hivi ndege zimepanda wapandaji
Fungua attachment hiyo
 
Attachments

  • ebb.jpg
    ebb.jpg
    36 KB · Views: 1,349
Hahaha kweli kabisa hao fastjet kule UK ni Easyjet msimamo wao ni huohuo sio hapa tu!
 
Huwa wana muda mfupi sana wa kusimamisha NDEGE yao kwenye sehemu ya kupandisha abiria. Wanafanya hivyo ili kukata gharama za Airport Charge na ndege kwa ujumla.

Nilishawahi kuona jamaa wamechelewa Turkish Air na saa moja kabla, geti lilifungwa. Ila sema Mungu bariki, kuna jamaa alikuwa na simu ya Boss mmoja wa hapo Airport na alipopiga, aliletwa dada mmoja, computer zikawashwa na sehemu ya check-in ikaanza kufanya kazi na wote waliochelewa wakasafiri.

Nilishawahi kusikia kuwa Jamaa alipanga kumzika mwenzake. Alikuwa kaagiza jamaa amtafutie ndege ya kusafirisha abiria ya kukodisha na jamaa akapata ndege na baada ya makubaliano, jamaa akalipa. Yule jamaa wa kwanza akawa huku ameshalipwa pesa na wateja na ndege kashapata ila yeye hakumlipa aliyelipia gharama za ndege na kukodisha. Akapanga kuondoka kimya kimya bila kulipa.
Basi asubuhi wakiwa wameshasimama kwenye landing lane tayari kuruka, wakaona ndege inarudishwa sehemu ya kushushia abiria. Wakamwambia "baba hujalipa watu huku....." Alivyolipa kwa aibu wakamruhusu.

Kuna ndege ilimsubiri jamaa kama dadika 45 na jamaa mwenyewe ukimuona ni mfupi na mdogo kwa umbo ila ni MKUBWA sana kwenye mambo ya safari. Na hii ndege ilikuwa na ndege ya kawaida kabisa ambayo haitakiwi isubiri mtu.

Ubabe upo sana ila kama wewe ni FULANI, ni kweli itasimama hata Msata ili jamaa amsalimie kwanza baba na ndipo muendelee na safari. Hiyo ndege saa moja kabla, angelikuja mtu kama MIE HAPA, simu moja tu wanafungua milango na computer (just jocking)........

Ila kama upo safarini tayari, ndege lazima wakusubiri kidogo kwani gharama za kukutunza hotelini kama ni wao wamekuchelewesha ni kubwa sana. Ndiyo maana utaona hata wanaita watu wakiona kuwa umesha check-in ila hujaonekana bado kwenye ndege. Ila kuna tofauti sana kati ya mashirika makubwa na madogo. Ndiyo maana bei zinapishana sana na huduma kwa ujumla.
 
Unalipa 32000 au hata 100,000,kwenda kurudi kj na unachelewa???nyie ndio wapuuzi wote 8,mshafanya hilo daladala.basi la mkoa lenyewe halisubiri abiria itakua ndege.nawapa sifa hao staff maana wangewaendekeza nyie itakuwa taabu mtataka hata kutumiwa gari nyumbani kuwachukua na buku 30 zenu nyambaf.

Na vipi kuhusu emergency,umefiwa ama unaumwa taratibu zikoje maana fastjet hawajui wanachokiona hapo ww ukikata ticket ndo basi lazima usafiri?mbn Air tanzania wao wanarudisha 75%? Mzigo ni pungufu ya kg 5 zaidi ya hapo unalipia kila kg tsh elf 8 kweli ndo mnasema wabongo wasiseme??waweke bei zao vizuri watoe huduma bora kwa wateja wao!zijajua sheria za TAA zinasema kuhusu hawa jamaa!
 
  • Thanks
Reactions: RR
Wabongo ukiwachekea hawakawii kumwambia rubani asimame chalinze wanunue nazi za kwenda nazo moshi.

Tena watataka badala ya kutua kia, ndege iwe inashusha na kupakia njiapanda ya imo, kiboruroni nk.

wewe inaonekana uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo,jitahidi usafiri kwenye nchi zenye mwanga kidogo ubongo utapata mwanga

,delay kwenye airline yoyote ni kitu cha kawaida,wabongo wengi tumelakla sana,amkeni mtembee kidogo
 
Wabongo ukiwachekea hawakawii kumwambia rubani asimame chalinze wanunue nazi za kwenda nazo moshi.

Tena watataka badala ya kutua kia, ndege iwe inashusha na kupakia njiapanda ya imo, kiboruroni nk.
Hahahaha, najuuuta!
Mtoa mada, muambie mshkaji akate pressicionair, kwani ni nini bana?
Nikupe siri ya mambo ya reporting time, manake hata ndege zingine za bongo wanafanya hiyo. Ukizuka airport unataka kuondoka ya fasta muda usio wa safari yako wanakuambia ngoja tuone kama kuna wachelewaji. So unacheck in security kabisa, unakaa ndani. Ikifika on dot wanakupa nafasi unaambaa zako. Mie nilimdrop mtu airport na flinght yangu ilikuwa ni kama 6hours later nikaingia tamaa ya kwenda kuzurura ugenini, na wakaniondoa kihivyo (sio na fastjet, na nilishaitubu hiyo zambi)
 
wewe inaonekana uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo,jitahidi usafiri kwenye nchi zenye mwanga kidogo ubongo utapata mwanga

,delay kwenye airline yoyote ni kitu cha kawaida,wabongo wengi tumelakla sana,amkeni mtembee kidogo

mbona unataka kujifanya umetembea sana?
 
wewe inaonekana uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo,jitahidi usafiri kwenye nchi zenye mwanga kidogo ubongo utapata mwanga

,delay kwenye airline yoyote ni kitu cha kawaida,wabongo wengi tumelakla sana,amkeni mtembee kidogo

Hakuna airline inayokatalia mtu kusafiri akichelewa 10 minutes ya reporting time. Minimum check in ni an hour au an hour and 15 minutes kabla ya departure time. Unless uniambie mtoa mada hajui tafauti ya departure na reporting time. Zamani ilikuwa kama vindege vya zenj hata ukifika saa ya departure unaitwa kila speaker na ukireport tu unapata special clearance unawahi japo unachelewesha ndege. Mambo ya terrorism yameharibu kila kitu, hakuna special clearance adabu mfukoni.
 
Malalamiko juu ya fastjet lazma yawe mengi manake yanahusisha watu ambao hawana uzoefu wa kutumia ndege Sikonge. Umenichekesha manake uhuni huo nishauona kwenye airline moja sio ya tz, ati ndege imekuwa overbooked. Kumbe kuna mhuni kaja kapewa ticket chapchap, ilisababisha delay ya an hour nikabaki nashangaa.
Hiyo ya kutangaza tshs 32,000/= bila kutaja hidden costs ni yale yale ya kina vodacom kusema ni tshs 1 kwa sekunde, na masharti na vigezo kuzingatiwa. Hapo ikichajiwa kodi na sijui dk ya kwanza ina masharti yake ndo wanapokuvuna. Seriously unategemea usafiri kwa tshs 32,000/= kama ndege haitumii mafuta jamani!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom