Bro sio hoja ya kipuuzi km unavodhani,
Shida hapa ni uthubutu Mwl JK alilinda sehemu zote zenye madini ili tukishapata elimu tuchimbe wenyewe na kuuza wenyewe but sisi wenyewe tukalishwa maneno na wazawa ambao tayari walishapewa chao kinono na wazungu na kuwakalilisha kuwa sisi hatuwezi kuchimba wenyewe hata kwa miaka miaka 500 ijayo ok.Tukawaruhusu wachimbe wao nasi tukapewa mrahaba kiduchu sana wao wakibeba zaidi ya 97%.Huo ndo Ushindani unaoutaka? WIZI MTUPU?
MF;Tunaambiwa China na Wachina walijifungia nchini mwao wao wenyewe kwa zaidi ya miaka 50 wakijijenga wao bila msaada kutoka nje leo hii wako na tuko wapi?
Bro acha mawazo hayo penda nchi yako jenga nchi yako.
Ushindani ni mzuri sana ila je ni washindani wapi tunashindana nao?Wezi au Wazalendo?
Kumbuka figisu la gesi na Mengi ambapo Waziri fulani alisema Mengi hana ubavu katika umiliki wa vitalu kisa waziri ana mawazo ya kijidharau na kuwadharau Watanzania wenzie kwa kuwa keshaonja za bepari
Hujui kitu. Usimezeshwe ujinga.
Kwenye madini corporate tax ni 30%. Unayoongelea 3% ni mrabaha na wala siyo kodi. Na hiyo 3% ni on production siyo on profit.
Katika Dunia yote ni Zimbabwe pekee hutoza mrabaha wa juu kuliko mataifa yote. Wanatoza 7%. Canada na Australia ni 0%. Baadhi ya mataifa wanatoza 1 na 2%.
Tatizo la Watanzania wengi ni ujinga. Ni wajinga katika mambo mengi lakini wanajua sana kubwabwaja wakiamini kuongea sana hata kama hujui unachoongelea, ni uelewa.
Wachina katika Ulimwengu wa kujifungia hawakufika popote. Waliendelea kuwa maskini wa kutupwa. China ya leo ni matokeo ya mabadiliko makubwa waliyoyafanya miaka kama 17 iliyopita. Walibadilisha sera zao za uchumi ambapo waliruhusu uwekezaji mkubwa toka nchi za Magharibi. Na makampuni ya Magharibi yamewekeza heavily in China.
Vitu vingi ambavyo ni high tech toka China vinatengenezwa na makampuni ya Ulaya na America
Hata train ziendaso kasi, ni mradi wa Wajerumani ambao mpaka leo China inailipa Ujerumani ambayo ndiyo yenye tekinolojia hiyo.
China bila uwekezaji mkubwa uliofanywa na makampuni ya Ulaya, America na South Korea, ni tupu.
Kwa hiyo usidanganywe kwamba China imefanikiwa kutokana na kujifungia. China ya kujifungia waliishia wote kuvaa nguo zenye viraka matakoni na magotini na mwisho hawakutoka na chochote cha maana.
Kihistoria China ilikuwa juu kimaendeleo kupita Japan lakini kutokana na mifumo yao mibaya ya kusimamia uchumi, China iliachwa mbali na Japan beyond comparison. Hali hiyo ni sawa pia kwa South Korea na North Korea