FastJet rekebisha hili: Malipo ya Ticket kwa Mpesa, Tigopesa na AirtelMoney

FastJet rekebisha hili: Malipo ya Ticket kwa Mpesa, Tigopesa na AirtelMoney

Ozzie

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2007
Posts
3,217
Reaction score
1,261
Mimi ni mmojawapo wa wahanga wa malipo ya ticket za FastJet kwa simu. Kuna wakati unaweza fanya booking ya ticket na kupewa reference number na expiry time ambazo pindi ukilipia booking husika, utashangaa kupata majibu kwamba ile booking imesha expire, japo upo ndani ya muda.
Shida kubwa hutokea katika ufuatiliaji wa pesa ambazo zimelipwa kwa njia ya simu wakati ticket ime expire (Hapa nazungumzia zaidi Mpesa). Kuna namba ya FastJet hutolewa na customer care Vodacom ili muathirika awasiliane na watu wa FastJet kwa ajili ya kurejeshewa malipo huku nao pia 'wakifanya mawasiliano na wahusika huko FastJet'.
Kwa masikitiko nimewasiliana na namba husika mara kadhaa usiku kwa matatizo yanayofanana. Mara nyingi simu hukatwa makusudi au kutopokelewa kabisa. Ikipokelewa kuna dada husikika moja kwa moja akiomba apigiwe simu muda wa kazi. Sasa huwa nashangaa kama simu inatakiwa itumike muda wa kazi tu, kwanini inakuwa hewani? Bahati mbaya huduma yao ya booking inafanyika 24/7 lakini ukiwa na shida hakuna wa kutatua. Huu ni uswahili sana...
 
Pole sana mkuu, hio lazima inakera mno! Pole sana endelea kuwakomalia
 
Ndio maana Kenya hawaitaki fastjet , kwa mambo ya kipuuzi kama haya
 
Back
Top Bottom