Fastjet transport.. Ni kweli imeleta hofu kwa precision air na atcl..?

acha kuropoka wewe...nilitaka kubook safari ya one week ahead...sasa hiyo zimamoto inatoka wapi?? au nawe unaandika tujue nawe umo jf???
Pole pole mtawa mwenzangu, punguza jazba.
 
acha kuropoka wewe...nilitaka kubook safari ya one week ahead...sasa hiyo zimamoto inatoka wapi?? au nawe unaandika tujue nawe umo jf???

Kiongozi, one week sio 'mapema' hata kidogo. Wetu wame-book mwezi June 2013 na bei ni powa kabisa. Taratibu tu Watanzania tutajua 'early' maana yake nini, na zimamoto nini and soon tutakuwa kama wajerumani wanaobook holidays miaka 2 kabla. Development.... hehehehehee....
 
Precision ni janga kwa wasafiri, mwezi wa7 nilinunu return ticket to mza from kia for 410000 utafikiri nakwenda Dubai, tar 27 mwezi uliopita nimenunua return ticket for the same route for 370000. Wao watafute jinsi ya ku swim along this strong wind. Waliweza kuziondoa/kuziuma kampuni zingine zilizopita kwa sababu business model ya makampuni hayo ilikuwa sawa na wao. Fastjet wao ni low cost model lazima itawatesa sana ,
 

umeongea vizuri sana,chukua like!
 
Reactions: FJM


naona hapo mambo ya "nguruwe pitaaaa,kwangu haramu weweee,sina mkuki mieee,ala lalala laaaaa laaaaa..."
 
Hata kwa sisi, tusio kua na uwezo wa laki tatu sasa ivi na sie tunapanda pipa kwa 43 elfu tu jamani.
 
imeleta hofu haswaa!mimi japo sio mpandaji wa ndege lakini nawaombea sana kwa mungu,ikiwezekana sio tu iwe cheap,hata isafirishe watu bure.
 
imeleta hofu haswaa!mimi japo sio mpandaji wa ndege lakini nawaombea sana kwa mungu,ikiwezekana sio tu iwe cheap,hata isafirishe watu bure.

Ha ha ha.. Ombi lako lipate kibali Mkuu..
 

Kama hawana bei nafuu kwa nini unatafuta tickets zao? Mimi nashauri uende na Precission tu mtu wangu. Wewe huwezi kuona kwamba ticket zimejaa kwa sababu watu wengi wanazikimbilia? Kwa nini wanazikimbilia? Kitu gani ambacho hawa jamaa wanacho ambacho kule kwingine hakipo hadi wajaze kila wakati?

Wala hunasababu ya kuwaghadhabikia na kuwaita waongo kwa kuwa umekosa ticket kwao. Kama wewe huhitaji luxury ya dk 40 ni kwa sababu ni wewe. Lakini wapo watu ambao hata ingekuwa ni dk kumi anataka awe katika luxury. Na isitoshe hata hiyo luxury hujataka kusema ni sh ngapi.

Ni vizuri ukawa mwunwana na ukakubali ukweli kwamba they are more competitive ndiyo maana ticket zao zinakuwa shida kuzipata. Na ujua kwamba pia kuna watu wa classes anuai. Usitake watu wote wawe sawa na wewe ambaye huoni umuhimu wa luxury kwa dk 40.


Ningekuwa wewe ningewashauri waongeze ndege ili ticket ziwe nyingi badala ya kuwakashif kama nadithi ya "Sizitaki mbichi hizi".

Kama ni waongo kw anini precision wameanza kuhaha?

Waongeze competitiveness, na siyo kutafuta sympathy na kutaka kushawishi serikali ianze kuleta monopoly eti kufavor Local Aviation ambayo imeshindwa kupunguza tatizo la usafiri wa ndani na kufanya domestic flight kuwa highly expensive na kuwaacha Watanzania walio wengi wakiona usafiri wa n dege ni wa watu maalum pengine wafanyabiashara wakubwa na wafanyakazi wakubwa wa serikali na mashirika.

Nchi nyingi domestic flights huwa ni affordable siyo vile wanafanya hapa bongo!. Wajifunze ku compete kama wanataka kuendelea kuwepo. Hakuna kulia lia serikali iwatetee! LOH!
 
huyo msemaji wa precision hajui kazi yake au hajui
nini maana ya competition kwenye aviation industry
ieleweke wazi wao walidominate aviation industry

kwa muda mrefu sana na waka abuse their dominant position
kwa kuweka price kubwa boyond capacity ya Mtanzania wa kawaida

na pia ikumbukwe aviation industry world wide
ni free market kila mtu ana uhuru wa kupanga bei yake
kutegemea na garama zake za uendeshaji

na kamwe hawaruhusiwi makampuni ya ndege kupanga bei pamoja
au kampuni ingine kulalama mwenzie
ana bei ndogo ni ukosefu wa elimu

hii sio biashara ya mafuta wanaweza
kuanzisha cartel lakini sio aviation industry.
watanzania endeleeni kufaidi usafiri

nafuu wa fastjet na hiyo ndio bei
ilitakiwa kutozwa na precision tangu mwanzo.
kama fair competition wakiingilia watakuwa
wanaminize competition na ofkzoz ntawashangaa sana kwa hilo
 
Fastjet ni mkombozi wetu,mm mwenyewe 5.12.12,nimesafiri na fast jet dar to mwanza kwa 43elf tu,wakati precision ilikuwa mpk 280000 one way kwenda mwanza,mungu ijaalie fastjet idumu ili tuache kuibiwa na hawa mabepari wa precisin,wametunyonya miaka mingi sasa mwisho wao umefika.
 
zimejaa kweli watu washafanya booking kama miezi miwili ijayo.wakikuambia luxury ndo zimebaki ni kweli kwa sababu ndenge kubwa zina first class ambapo kwa fast jet kwa kuwa watu wanakimbilia unafuu hawatazipenda.
 

...it's Newtons 3rd Law of Motion...." Into every action there is equal and opposite reaction"....
 
Nimepanda Precisionair na ATCL mara nyingi tu but cijawahi kutoa pesa yangu ya mfukoni kununua ticket..! Ila kwa unafuu kama huu wa Fastjet.. nitatumia my own money kununua ticket.. Najua mpo wenye hela nyingi but kulipa return ticket kwa Tshs. 377,000/= wakati Nikikamata Dar Express return ticket haizidi Tshs. 60,000/= kwangu ni anasa ambayo cintokuja kuifanya..
 

Wala Precision wasiogope! Jumapili nimekuja Dar na ndege ya PW 415 ambayo ni boeing. Ilitoka Mwanza ikiwa imejaa tele! Cha kufanya ni Precision wajitahidi kwenda na wakati tu and they will compete with fastjet. Mbona nilishangaa ata ATC inapata na kujaza watu sasa sembuse Precision jamani?
 
Kweli kumekucha Tanzania, Low Cost Carrier (LCC) ziko dunia nzima. Tatizo hatupendi hesabu, Somo la hisabati limewatoka watu hapa. Ukipanda FastJet unalipia mzigo wako na huduma yeyote ukihitaji unalipia humo ndani. Lakini Precision haulipii mzigo tena kwani ulishalipia kwenye tiketi yako na huduma nyingine. Vigezo na msharti vinakua vimezingatiwa.
Hakuna kitu cha bei rahisi hapa, liko wazi kwamba viwanja vyenye uwezo wakupokea ndege kubwa viko vichache tu ambako ndege ndogo kama ATR ndio zinaweza kutua. Huu msimu wa sikukuu ukiisha tutajua mbivu na mbichi.
 

Kweli wewe ni Mwanahisa wa Precision,
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…