Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Septemba mwaka 2019, wakili Karume alisimamishwa kufanya kazi ya uwakili Tanzania Bara, maamuzi yaliyotolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na Ado Shaibu akipinga uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali kuteuliwa kimakosa na Rais Magufuli na kesi iliondolewa.
Mahakama kuu iliamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili ya mawakili kwa kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu ambae ndiye alikuwa wakili wa Ado Shaibu katika kesi hiyo.
Pia, soma=> Fatma Karume asimamishwa kufanya kazi za Uwakili
===
Akijibu hoja ya mdau kwenye mtandao wa twitter aliyemuomba akate rufaa dhidi ya uamuzi huo, Fatma amesema hatafanya hivyo kwa maelezo kwamba muamuzi wa rufaa yake sio huru.
"Ukiingia kwenye mapambano unahitaji kujua nani unapambana nae, kanuni za mpambano na uhuru wa muamuzi. Iwapo kanuni haziko wazi na muamuzi hayuko huru, huo sio mpambano bali upotevu wa muda. Hifadhi nguvu zako kwa mpambano unaoweza kushinda". Yalinukuliwa majibu ya Fatma Karume.
Pia, soma=> TLS: Kamati ya Maadili Haijahusika Kumuondoa Fatma Karume kwenye orodha ya Mawakili