Fatma Karume aondolewa kwenye orodha ya mawakili (Permanent removal), akutwa na hatia ya kukiuka maadili

Unaandika kwa hisisa na chuki tu. Yeye Karume ni mwanasheria, na amepata umaarufu huo kwa sababu ya taaluma yake ya sheria; sasa leo kama hakubaliani na mahakama, ambacho ndicho chombo kinachotoa haki kisheria, basi asipeleke kesi zake huko. Akishakubali kwenda kutaja kesi huko ina maana anakubali kuwa yuko pale kutafuta haki. Kwenda na kuanza kujifanya mjuaji ndiyo inamtokea puani sasa. Aliwahi kutoa vitisho fulani zamani kidgo ikabidi yule hakimu ajiotoe kwenye kesi na kuisababisha kesi ikae muda mrefu sana bila kusikilizwa kwa vile mahakimu wengine wote walikataa kuichukua. Hiyo ikawa ni kumtesa mteja wake ambaye alikuwa anataka shauri lake lisisikilizwe mapema, lakini lilichelewesha kwa takriban mwaka mzima kutokana na upuuzi wake. Yuko anaropoka kama vile hajui kuwa anaruhusiwa kukata rufaa iwapo hakubaliani na hukumu; ila uropokaji ndio anaotanguliza mbele kama vile amesoma sheria chini ya mti.

Bado hujatoa ushahidi wowote kuwa Lissu alishambuliwa na nani, ni maneno ya kujitungia kwa hisia na chuki tu. Zamani sana Profesa Jwani Mwaikusa alipigwa risasi na kuuwawa mchana kweupe na mpaka tunapoongea leo haijajulikana ni nani waliomshambulia. Ingekuwa ni leo hii ungesema pia kuwa ni serikali. Huwezi kujua kuwa mtu mropokaji namna hiyo huwa pia anatengeza maadui wengi huko huko mitaani.

Akwilina hakuuwawa kwa sababu zozote za kisiasa ilikuwa ni umamuzi mbaya wa askari mmoja katika kutuliza ghasia, lakini watu kama wewe leo mnalifanya jambo la kisiasa. Mara nyingi watu waliofilisika kisisasa hutafuta sababu nyingine zozote zile ili kuonekana wako relevant
 

..serikali inalaumiwa ktk tukio la Tundu Lissu kutokana na ukweli kwamba walinzi wa area D waliondolewa siku ambayo shambulizi lilitokea.

..kwasababu walinzi wa area D ni wa serikali, na wanaoweza kuwaondoa ni mamlaka za serikali, ndiyo maana tuhuma za kumshambulia Tundu Lissu zinaelekezwa kwa serikali.
 
Ushabiki maandazi wa Twitter matokeo yake ndio kama haya Victims wanazidi kuongezeka tu.

Membe anaonja joto ya jiwe,

Kafuatia Fatma.
 
Amevualiwa uwakili ila bado hatujawafahamu waliohusika kumvua huo uwakili

Walivyofanikiwa awataendelea kuwavua mawakili wengine wasiokubaliana na wanavyoamini wao?

Waliosoma sheria wananafasi gani kuilinda taaluma hii isidharaulike?

Walienguliwa WANASHERIA watumishi wa umma kupractice wakatulia, Leo wameanza kupokonywa vyeti katika nchi inayoamini vyeti na leseni. Tujipange
 
Tayari TLS wamejitoa..serikali ovu lazima ibaki na aibu..viva Shangazi

Ipo siku watu kama akina Kabudi hawatakuwa na cha kujieleza huko mbeleni maana ni wanasheria ila wapo upande wa uovu kuhamasisha uovu na matumbo yao
 
Nimeota TL rais Shangazi waziri Sheria na katiba
Tundu Lissu naye zamu yake ya kuondolewa kwenye orodha ya mawakili wa Tanganyika inafuata mara tu baada ya 28 October. Makosa yao yanafanana. Tena ya Lissu ni makubwa zaidi. Kamtukana hadi Jaji Mkuu na Rais wa JMT. Wote ni political activists, hali inayowaondolea sifa ya kuwa wakili wa mahakama za Tanganyika. Ulishaona wapi rais wa nchi akawa pia wakili wa mahakama za nchini kwake. Kitendo cha kugombea urais kinamfuta permanently kuwa wakili wa mahakama hata kama atashindwa kwenye uchaguzi huu (something very certain).
 
Maelezo tosha na ya kueleweka. 👍👍
 
Ushabiki maandazi wa Twitter matokeo yake ndio kama haya Victims wanazidi kuongezeka tu.

Membe anaonja joto ya jiwe,

Kafuatia Fatma.
Majibu ya huu ufedhuli mnaoufanya mtayapata tarehe 28/10/2020.

Mnazidi kutufanya wananchi tumuelewe zaidi Tundu Antiphas Lissu anaposema Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu!

Tukutane Oktoba 28.
 
Kwa hiyo wewe kilaza wa Lumumba tuambie Nani Alimpiga risasi Tundu Lissu???

Kwa nini hadi leo polisi hata Lissu tu hawajamuhoji??? Kwa nini walinzi kwenye nyumba za Viongozi alikokuwa anakaa Lissu waliondolewa??? Kwa nini mlimnyima matibabu Lissu???
 
Majibu ya huu ufedhuli mnaoufanya mtayapata tarehe 28/10/2020.

Mnazidi kutufanya wananchi tumuelewe zaidi Tundu Antiphas Lissu anaposema Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu!

Tukutane Oktoba 28.
Hakuna aliyemtuma akaikashifu ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, kuidharau mahakama ??

Ukiona unasifiwa sana Twitter jiandae kwa anguko la aibu.

Membe anasikilizia utamu huko aliko, alikuwa akijazwa maneno kuwa ni Rais , sasa anahutubia viwanja vitupu tu.
 
Amemkashifu vipi mwanasheria mkuu wa serikali??? Ameidharau kivipi mahakama????


Amini nakwambia Kabla mwaka huu haujaisha Fatma karume anaenda kurudishiwa nafasi zake zote na anapata nyingine zaidi.

CCM na watu wenu fanyeni udhalimu wenu wote ila jueni tu kuwa mwisho wenu ni October 28 mwaka huu.
 
Anayefuata kufutwa kwenye orodha hiyo ni Lissu, baada ya kushindwa vibaya Uchaguzi Mkuu.

Amedharilisha TLS wakati wa kutafuta udhamini na kampeni za Urais. Akitambua kuwa alikuwa Rais wa TLS alipaswa kuheshimu Sheria, Kanuni na Taratibu za uchaguzi Tanzania. Isitoshe amekuwa akitoa matamshi yenye kudharilisha watumishi wa Mahakama, kama mihimili unaojitegemea, ambao yeye pia ni mhusika.
 
Ukitaka maendeleo kwenye nchi yoyote hasa Africa moja demokrasia,mbili vyombo vya habari viwe huru,bunge liwe huru ,tatu vyama vya wafanyakazi vyote viwe huru,mahakama iwe huru kinyume cha hayo hapo juu nchi inakuwa kwenye matope ya umaskini wa kutupwa kama Tanzania yaani hivi nchi hii imefikia mahali paa mwanaume kumwogopa mwanamke yaani Fatuma Karume hivi ni kweli !!?Yaani wanaume wenye kende tuliotahiliwa tumeshindwa kumjibu huyu dada kwa hoja lakini tunakimbilia kujificha gesti hivi ni kweli ?Wanaume wale kama akina Paulo,Goliati ,Zebedayo mpo wapi? Ifikapo 2050 watakuwa wengi sana kama fatuma hivi wanaume mtajificha wapi ?Aisee tujipe pole watanzania !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…