Fatma Karume aondolewa kwenye orodha ya mawakili (Permanent removal), akutwa na hatia ya kukiuka maadili

Kikao cha kamati ya maadili ya Mawakili kilichokaa leo tarehe 23/9/2020 kimemkuta na hatia ya kukiuka maadili kwa kiwango cha juu, wakili Fatma Karume mwenye roll namba 848 na hivyo kuamuru jina lake liondolewe (permanent removal) katika orodha ya mawakili Tanganyika.

September mwaka 2019, wakili Karume alisimamishwa kufanya kazi ya uwakili Tanzania Bara, maamuzi yaliyotolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na Ado Shaibu akipinga uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali kuteuliwa kimakosa na Rais Magufuli na kesi iliondolewa.

Mahakama kuu iliamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili ya mawakili kwa kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu ambae ndiye alikuwa wakili wa Ado Shaibu katika kesi hiyo.

Pia, soma=> Fatma Karume asimamishwa kufanya kazi za Uwakili

===
Akijibu hoja ya mdau kwenye mtandao wa twitter aliyemuomba akate rufaa dhidi ya uamuzi huo, Fatma amesema hatafanya hivyo kwa maelezo kwamba muamuzi wa rufaa yake sio huru.

"Ukiingia kwenye mapambano unahitaji kujua nani unapambana nae, kanuni za mpambano na uhuru wa muamuzi. Iwapo kanuni haziko wazi na muamuzi hayuko huru, huo sio mpambano bali upotevu wa muda. Hifadhi nguvu zako kwa mpambano unaoweza kushinda". Yalinukuliwa majibu ya Fatma Karume.
Naye amezidisha chumvi, kiukweli Fatma anatabia ambazo si za kiwakili sijui anavuta kitu
 
Si akafanyie kazi za uwakili kwao Zanzibar au kwenyewe kesi za maana hazipo bali ni kesi za kuibiana madafu? Ukijifanya mjuaji kupitiliza hayo ndio matunda yake
Hawa mawakili wasomi wa Tanganyika wakati wanampa urais wa chama chao sijui ubongo wao walikuwa wameuweka wapi!
 
Whenever the fight is for the right course count me in....
4the1st time I like your comment.
Thank you!

If we don’t use this chance this October to remove this guy from the top post, Tanzania will be in total disarray in next 5 years. He enjoys to make people suffer.
 
Huyu binti ana asili yabm kisomali, ana Nasaba na Marehemu Mzee Diria, aliyekuwa waziri wa mambo ya njee serekali ya mwinyi.

Wasomali ni majasiri na hawana mchezo, hapo wamechokoza nyuki
 
Thank you!

If we don’t use this chance this October to remove this guy from the top post, Tanzania will be in total disarray in next 5 years. He enjoys to make people suffer.
Mmechelewa mnamuondoaje kwa mikakati mfu, badala ya kuwekeza kutafuta wabunge na kuwapa support mnahangaika kuchota maji ya kisima kuhamishia baharini.Upinzani wa Tanzania majanga.
 
Huyu mama kama alivyo Lissu ni mawakili wa kiharakati ndiyo maana amwekuwa ni waropokaji. Wewe wakili msoni unaweza kuimbia mahakama maneno hayo?
1600867409358.png

Yaani anaitishia mahakama anajifanya yeye ni mjuaji zaidi ya mahakimu? Hajui kuwa mawakili huwaita mahakimu "Your Lordship?"
 
Kila anae ongea ukweli CCM lazima wamfanyie figisu ili aharibikiwe. Huyu mama kosa lake lilikua ni kutetea na kuongea maovu yanayofanywa na serikali.

Lissu asiposhinda uchaguzi huu, basi na yeye atafanyiwa figisu ili aondolewe kwenye Advocate Roll. Ila Tundu Lissu akiwa Rais basi Fatma Karume atakuwa Waziri Wa Sheria au Mwanasheria Mkuu Wa Serikali (Hapa ndio mahakama na wanasheria wanaotumikia na kuwaabudu CCM watakapo juta).
Bado Lissu mnampa sifa sawa na mlivyofanya kwa Mange na Membe, Lissu mtaachana naye 28/10 mtakapojikuta hamna sifa za kupiga kura.Mlihamasishwa kujiandikisha mkadharau
 
Nadhani Fatuma Karume asingekuwa Mzanzibari na mtoto wa Rais; watu wasiojulikana wangekuwa wameshamnymazisha kwa njia tofauti na hizi zinazotumika sasa! Chuki dhidi yake imepitiliza; ni kama kuna watu wanamuona hastahili kuwa hai! Inawezekanaje mtu kunyang'anywa kirahisi tu haki ya kufanya kazi ili ajipatie riziki yake bila hata kupewa nafasi na muda wa kujirekebisha? Je, huu ndio mwelekeo mpya wa nchi yetu kwa siku zijazo chini ya ccm?
 
Huyu mama kama alivyo Lissu ni mawakili wa kiharakati ndiyo maana amwekuwa ni waropokaji. Wewe wakili msoni unaweza kuimbia mahakama maneno hayo?
View attachment 1578326

Yaani anaitishia mahakama anajifanya yeye ni mjuaji zaidi ya mahakimu? Hajui kuwa mawakili huwaita mahakimu "Your Lordship?"

Katiba ametunga Binadamu /ina Makosa/inafaa irekebishwe na ndio sababu baadhi ya Vifungu hubadilishwa kutokana na mahitaji na wakati unataka nini.Haya maneno yake kama yalionekana kuitishia Mahakama ilitakiwa kwa waliotoa maamuzi wajiridhishe na hayo matisho yapo ktk mstari upi.

Mwenyewe ameshakiri kuwa yupo mwenye nguvu zaidi juu ya hili swala ,ndio sababu Sheria zinageuzwa kichwa chini Miguu juu.Nna mkubali sana Mtu mwenye msimamo usio yumba ,nyeupe ataisema ni nyeupe vivyo hivyo kwa nyeusi ataisema hivyo hivyo.

Yalio mkuta Mh Lissu ni mfano tosha na Mungu huyu huyu (wa wema na wabaya) aliamua kuwavua Nguo wabaya waliotaka kumtoa Roho yake kule Dodoma,Sheria mbovu zinazompa Mtu au kikundi cha Watu umungu Mtu hazifai na zipo kinyume kabisa.Inawezekana leo yame mtokea Mh Lissu /Fatma Karume /Akwilina (R.I.P) hatujui anae fuatia.

Chunga sana Ahmali yako Mkuu hapa Duniani.
 
Sidhani kama anahitaji msaada kutoka kwa mtu yeyote; alishasema anaweza wakati wowote kurudi Uingereza kufanya kazi ya uwakili. Pengine wenye mamlaka wamelenga kumsukuma kufikia uwamuzi huo! Very insecure!
 
Katiba ametunga Binadamu /ina Makosa/inafaa irekebishwe na ndio sababu baadhi ya Vifungu hubadilishwa kutokana na mahitaji na wakati unataka nini.Haya maneno yake kama yalionekana kuitishia Mahakama ilitakiwa kwa waliotoa maamuzi wajiridhishe na hayo matisho yapo ktk mstari upi.

Mwenyewe ameshakiri kuwa yupo mwenye nguvu zaidi juu ya hili swala ,ndio sababu Sheria zinageuzwa kichwa chini Miguu juu.Nna mkubali sana Mtu mwenye msimamo usio yumba ,nyeupe ataisema ni nyeupe vivyo hivyo kwa nyeusi ataisema hivyo hivyo.

Yalio mkuta Mh Lissu ni mfano tosha na Mungu huyu huyu (wa wema na wabaya) aliamua kuwavua Nguo wabaya waliotaka kumtoa Roho yake kule Dodoma,Sheria mbovu zinazompa Mtu au kikundi cha Watu umungu Mtu hazifai na zipo kinyume kabisa.Inawezekana leo yame mtokea Mh Lissu /Fatma Karume /Akwilina (R.I.P) hatujui anae fuatia.

Chunga sana Ahmali yako Mkuu hapa Duniani.
Tanzania baada ya uchaguzi wa 2015, tulipoteza busara ya kuoeana haki na kufuata katiba. Ninachoogopa sasa ni huyu Dada akaulizwa kuhusu Uraia wake, japokuwa nj mtoto wa Raisi msataafu. Kwa mizizi yao ina michanganyiko mingi, inasemekana wana Ungazija, Maliwi, Usomali, ushirazi. Japokuwa idadi kubwa ya wazanzibari wamechanganya sana
 
Sasa mbona.Madam,anaonekana.kuridhika kirahisi mno na maamuzi Yale????!
 
Kikao cha kamati ya maadili ya Mawakili kilichokaa leo tarehe 23/9/2020 kimemkuta na hatia ya kukiuka maadili kwa kiwango cha juu, wakili Fatma Karume mwenye roll namba 848 na hivyo kuamuru jina lake liondolewe (permanent removal) katika orodha ya mawakili Tanganyika.

September mwaka 2019, wakili Karume alisimamishwa kufanya kazi ya uwakili Tanzania Bara, maamuzi yaliyotolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na Ado Shaibu akipinga uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali kuteuliwa kimakosa na Rais Magufuli na kesi iliondolewa.

Mahakama kuu iliamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili ya mawakili kwa kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu ambae ndiye alikuwa wakili wa Ado Shaibu katika kesi hiyo.

Pia, soma=> Fatma Karume asimamishwa kufanya kazi za Uwakili

===
Akijibu hoja ya mdau kwenye mtandao wa twitter aliyemuomba akate rufaa dhidi ya uamuzi huo, Fatma amesema hatafanya hivyo kwa maelezo kwamba muamuzi wa rufaa yake sio huru.

"Ukiingia kwenye mapambano unahitaji kujua nani unapambana nae, kanuni za mpambano na uhuru wa muamuzi. Iwapo kanuni haziko wazi na muamuzi hayuko huru, huo sio mpambano bali upotevu wa muda. Hifadhi nguvu zako kwa mpambano unaoweza kushinda". Yalinukuliwa majibu ya Fatma Karume.
Baada ya 28 10 2020 watamrudisha nakumuomba radhi
 
Back
Top Bottom