Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Lakini pia nadhani uanaharakati wake umechangia.Duh!, Hiyo inatosha kumzuia ku practice?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini pia nadhani uanaharakati wake umechangia.Duh!, Hiyo inatosha kumzuia ku practice?
Na mii nikitaka niseme hivyohivyoMaagizo kutoka juu.
Unajua Uzalendo lkn Maadili hujui...Mmonyoko wa maadili, na inasikitisha sana kwa mtu unayejitambua kuandika kauli mbaya kama hii. I hope kizazi kama wewe mnapaswa mfundishwe uzalendo.
Kikao cha kamati ya maadili ya Mawakili kilichokaa leo tarehe 23/9/2020 kimemkuta na hatia ya kukiuka maadili kwa kiwango cha juu, wakili Fatma Karume mwenye roll namba 848 na hivyo kuamuru jina lake liondolewe (permanent removal) katika orodha ya mawakili Tanganyika.
September mwaka 2019, wakili Karume alisimamishwa kufanya kazi ya uwakili Tanzania Bara, maamuzi yaliyotolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na Ado Shaibu akipinga uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali kuteuliwa kimakosa na Rais Magufuli na kesi iliondolewa.
Mahakama kuu iliamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili ya mawakili kwa kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu ambae ndiye alikuwa wakili wa Ado Shaibu katika kesi hiyo.
Pia, soma=> Fatma Karume asimamishwa kufanya kazi za Uwakili
===
Akijibu hoja ya mdau kwenye mtandao wa twitter aliyemuomba akate rufaa dhidi ya uamuzi huo, Fatma amesema hatafanya hivyo kwa maelezo kwamba muamuzi wa rufaa yake sio huru.
"Ukiingia kwenye mapambano unahitaji kujua nani unapambana nae, kanuni za mpambano na uhuru wa muamuzi. Iwapo kanuni haziko wazi na muamuzi hayuko huru, huo sio mpambano bali upotevu wa muda. Hifadhi nguvu zako kwa mpambano unaoweza kushinda". Yalinukuliwa majibu ya Fatma Karume.
Makosa yake ni yepi? Huyu mama mwaka huu analo, kule Imma advocates wamemtimua na huku nako pia
Kama ni sehemu ya Tanzania kwa nini huyo Fatma Karume alihoji kwamba iweje Mgombea u-Rais wa Zanzibar achaguliwe Dodoma?Unasahau kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania?
Kwani JPM ataapishwa tarehe ngapi?Asubiri rais mpya, rais watu aingie ofisini.
Mengi yaliyo fyongo na sheria fyongo kama za yule rubani wa Chopa zitakwenda naye kupumzika Chatto.
Ni jambo la kufurahisha kuwa Tanzania mpya iko njiani!
Hawajaweka wazi makosa yake?
..hivi hawezi kuchallenge decision?
Tuko wapi "Uhuru na Haki"?Kikao cha kamati ya maadili ya Mawakili kilichokaa leo tarehe 23/9/2020 kimemkuta na hatia ya kukiuka maadili kwa kiwango cha juu, wakili Fatma Karume mwenye roll namba 848 na hivyo kuamuru jina lake liondolewe (permanent removal) katika orodha ya mawakili Tanganyika.
September mwaka 2019, wakili Karume alisimamishwa kufanya kazi ya uwakili Tanzania Bara, maamuzi yaliyotolewa na Jaji Feleshi kwenye kesi iliyofunguliwa na Ado Shaibu akipinga uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali kuteuliwa kimakosa na Rais Magufuli na kesi iliondolewa.
Mahakama kuu iliamuru Fatma apelekwe kamati ya maadili ya mawakili kwa kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu ambae ndiye alikuwa wakili wa Ado Shaibu katika kesi hiyo.
Pia, soma=> Fatma Karume asimamishwa kufanya kazi za Uwakili
===
Akijibu hoja ya mdau kwenye mtandao wa twitter aliyemuomba akate rufaa dhidi ya uamuzi huo, Fatma amesema hatafanya hivyo kwa maelezo kwamba muamuzi wa rufaa yake sio huru.
"Ukiingia kwenye mapambano unahitaji kujua nani unapambana nae, kanuni za mpambano na uhuru wa muamuzi. Iwapo kanuni haziko wazi na muamuzi hayuko huru, huo sio mpambano bali upotevu wa muda. Hifadhi nguvu zako kwa mpambano unaoweza kushinda". Yalinukuliwa majibu ya Fatma Karume.
Aende kwa kina Amsterdam.Zanzibar hakuna kesi za maana
Natamani Mungu atusaidie watz hili litokee yaani Lissu awe rais wa Jamhuri ya Tanzania tutakuwa tumepata uhuru wa kweliKila anae ongea ukweli CCM lazima wamfanyie figisu ili aharibikiwe. Huyu mama kosa lake lilikua ni kutetea na kuongea maovu yanayofanywa na serikali.
Lissu asiposhinda uchaguzi huu, basi na yeye atafanyiwa figisu ili aondolewe kwenye Advocate Roll. Ila Tundu Lissu akiwa Rais basi Fatma Karume atakuwa Waziri Wa Sheria au Mwanasheria Mkuu Wa Serikali (Hapa ndio mahakama na wanasheria wanaotumikia na kuwaabudu CCM watakapo juta).
Ndiyo kwani unajifanya hujui si wametekeleza maagizo kutoka juu kwa jiwe wenuCCM ndio wamemfuta uwakili?!
Alikuwa na kizuizi?!Rasmi sasa kujiunga na chama chochote cha siasa
Sio uongo mbona yule jamaa anapwaya kweny ile nafasi alowekwaKosa lake ni kumshambulia Mwanasheria Mkuu wa serikali kuwa hana sifa hiyo na kwamba Rais alikosea kumteua.
Hao ni miungu watu utawasemaje mkuu hawaguswi haoKama hii sheria / kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu ipo basi haifai na ifutwe..., haya mambo ya kusema taasisi fulani / watu fulani hawawezi kushambuliwa au kukosolewa ni nzuri mpaka pale taasisi hizo zinapokosea au kufanya makosa...., sasa hapo ni nani wa kuwashambulia na kuwakosoa?