The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
Mkuu, watu walizuiwa kuvaa T-shirt za Lissu na kumuombea kiwa mahututi hospital. Ushaona wapi hiyo ....!! Kwa nini hakuna Mbunge yeyote wa CCM alikwenda kumtembelea Lissu Nairobi ... Ndiyo maana nasema all the circumstantial evidence zinapoint upande fulani.T-Shirt za Lissu zilianza baada ya Lissu kuwa amepigwa risasi na ndipo watu wakawa wanamwombea apone, siyo kwamba alipigwa baada ya watu kuwa wanamwombea. Halafu watu hawakukamwata ilikuwa ndiyo hii ya kuzusha tu, kwani ilibidi Kamanda wa polis atoe tamko kuwa huo ni uzushi tu.
Ni kweli aliwahi kusema kuna watu wanamfuatilia lakini ali-conclude kuwa ni usalama wa taifa bila kuwa amefanya uchunguzi wowote. Zaidi zaidi alitangazia vyombo vya habari bili kuripoti polis kuwa anadhani kuna majambazi wanamfuatilia. Alichanganya sheria na siasa, na wakati mwingine hiyo unakuwa unatoa opportunity zaidi kwa hao majambazi . Zamani kidogo Mwakyembe naye aliwahi kuripoti kufuatiliwa na watu wakitaka kumwua lakini alipeleka taarifa hiyo polisi kwa mkuu wa polis wakati huo akiitwa Mangua (nadhani), ingawa baadaye akalishwa sumu.
Ujambazi bado upo nchini lakini tunapofikia kusema kila ujambazi unafanywa na serikali tunakuwa tunatoa nafasi kwa ujambazi kuendelea kwa vile wanajua kuwa hawatatafutwa, na ukishaihukumu serikali kwa ujambazi huo, ina maana unaondoa au unapunguza sana ushirikiano na serikali hiyo.
Ni kweli kabisa ujambazi kama huo unaweza kufanywa na watu binafsi ... lakini kitendo cha vyombo vyetu kushindwa kujishugulisha kupeleleza eti wakidai wanamsubiri Lissu, inatia shaka kama kweli wana nia hiyo. Ina maana kama Lissu na dereva wangekufa huo ndo ungekuwa ni mwisho wa upelelezi wao!!