Fatma Karume: Yaani leo nimethibitisha Adelardus (AG) hajui Katiba, anadai Serikali ina mihimili mitatu na yeye ndie anasimamia yote

Fatma Karume: Yaani leo nimethibitisha Adelardus (AG) hajui Katiba, anadai Serikali ina mihimili mitatu na yeye ndie anasimamia yote

Acha uhuni ,umeandika wewe kule juu....alafu kumbuka Spika anatokana na chama ambacho Rais ndiye mwenyekiti ata kama apigiwi kura za kua Mwenyekiti.
Chama tawala kinapitisha jina la spika alafu anachaguliwa na Bunge. Acha kuchemka ...
 
Serikali ni mhimili mmoja kati ya 3,ana maanisha nini?
Serikali ina mihimili 3,Executive judiciary and Legislature, kosa liko wapi? Maana ni serikali moja iliyojigawa katika mihimili mitatu.
Chadema imejaa wavuta bangi na wanywa konyagi. Upuuzi kama huu sio wa kushabikia.
Aiseeee Kweli Mtaji wa CCM ni WAJINGA yaani Serikali ina mihimili mitatu na mmoja wapo ni Serikali? Nimeamini ndani ya CCM wamejaa UTOPOLO na nyie ndio washauri hapo LUMUMBA.
 
Aiseeee Kweli Mtaji wa CCM ni WAJINGA yaani Serikali ina mihimili mitatu na mmoja wapo ni Serikali? Nimeamini ndani ya CCM wamejaa UTOPOLO na nyie ndio washauri hapo LUMUMBA.
Kasome doctrine of separtion of powers uondoe ujinga. Usidhani kupost Jf ndio kujua mambo. Unaweza ukawa unapost ila unafikiri kwa kutumia makalio kama wenzako.
 
Kasome doctrine of separtion of powers uondoe ujinga. Usidhani kupost Jf ndio kujua mambo. Unaweza ukawa unapost ila unafikiri kwa kutumia makalio kama wenzako.
Hicho unachokitetea ni sawa na kusema Hawa ana watoto watatu ambao ni Hadija, Janeth na Hawa Mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hicho unachokitetea ni sawa na kusema Hawa ana watoto watatu ambao ni Hadija, Janeth na Hawa Mwenyewe [emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo ni kukosa elimu. Ungekuwa umeelimika usingeumiza kichwa. Maana mlishaambiwa serikali ina mihimili mitatu na mmoja umejisimika zaidi sababu ndio inalipa gharama za mihimili yote.
Huko ufipa mmejazana wavuta bangi na wanywa konyagi.
 
Chama tawala kinapitisha jina la spika alafu anachaguliwa na Bunge. Acha kuchemka ...
Chama chini ya Mwenyekiti ambae ni Rais aaaah
Alafu Mwenyekiti ambae ni Rais anamwambia Spika awashughurikie huko mdani aaah....SPIKA ANATEULIWA NA RAIS AMBAE NI MWENYEKITI
 
Tatizo ni kukosa elimu. Ungekuwa umeelimika usingeumiza kichwa. Maana mlishaambiwa serikali ina mihimili mitatu na mmoja umejisimika zaidi sababu ndio inalipa gharama za mihimili yote.
Huko ufipa mmejazana wavuta bangi na wanywa konyagi.
Wewe ambaye umepata elimu unachukulia kitu kama kilivyo/kinavyofanywa na sio kama inavyotakiwa kuwa.

Hiyo Serikali ina matawi na sio mihimili. Lumumba inatakiwa iwape elimu watu wake na waelimike ndipo wawape simu za kutumia.
 
Mwanasheria mkuu yupo sahihi, huyo Fatuma karume kapuyanga hapo. Hata shuleni somo la Civics tu inafundishwa matawi ya serikali ni matatu, ambayo ni excutive(serikali kuu inayohusika na utrndaji wa serikali nzima), Judiciary(Mahakama) na Legislature(Bunge).

Haya kwa pamoja huitwa branches of government(matawi ya serikali). Mtoto wa kidato cha tatu tu anaweza kukufafanulia kuhusu hilo, sikutarajia mwanasheria kama yeye angeweza kukuruouka tu.

Excutive ambayo anaisemea ni serikali nzima, anakosea sana. Lile ni tawi la serikali tu linahusika na utendaji mkuu, na si kwamba linabeba serikali nzima.

Sitarajii na watu humu ambao mmemaliza hata vidato vyote, mkakaa na kulibishia suala hili. Wakati huko mlifindishwa serikali ni nini, na matawi ya serikali ni yapi. Hata ukiingia kwenye article zenye kuijadili serikali ya Tanzania. Zinaonesha hilo
Kwenye books of accounts za mzazi wako Ada aliyotumia kukusomeshea inabidi aiweke kwenye Loss
 
Government?

The group of people with the authority to govern a country or state; a particular ministry in office.

Na ukisikia nchi mmepinduliwa, kinachopinduliwa ni government , ni watu walio shika madaraka tu, na pale tu tunapo sema serikali inavunja sheria au inawaonea wananchi au wanasiasa, maana yake ni viongozi wenye mamlaka.

Wengi wanavyo fahamu police ni government, au bunge au mahakama, hivi ni vitu tofauti, lazima tuelewane bwana. Nyie wanasheria muwaelimishe watanzania
 
There you are! Kumbe wampata..Kilangi ni gwiji kwenye International Law lakini hna credentials za kuwa AG. Source kutoka kwa insider: yeye mwenyewe alishangazwa kwa kuteuliwa kuwa AG. Hii nchi ina matatizo sana!!!
Tusidanganyane; Waikili yeyote anaweza kuwa AG haijalishi kabobea kwenye nini.

Kusema Killangi kabobea kwenye international law haiwezi kuwa sababu ya kumdisqualify kuwa AG.

International law ni public law na hauwezi kubobea kwenye international law halafu uwe poor kwenye Municipal law ambayo ni mandatory kuliko hiyo international law kwenye vyuo vingi haikuwa mandatory course huko nyuma.

Itoshe kusema kuwa huenda hajui tofauti ya serikali na dola au aliteleza lakini tusihamishe goli kwa kusema amebobea kwenye international law nakataa.
 
Kwa maana ya uwakilishi wa kisheria nje ya nchi bila kujali inahusu bunge, mahakama ama executive atawakilisha AG.

Nimekosea mkuu?

Naomba nijifunze na isichukuliwe kama hoja.

Thanks

Nadhani bado itategemea uwakilishi huo ni kwa ajili ya nini. Nadhani kwa vile mwakilishi wa dola nje ya nchi ni serikali (k.m. mahakama na Bunge hawana uwakilishi nje tofauti na balozi zetu ambazo ni sehemu ya serikali) basi AG atapewa jukumu la kuwakilisha mihimili mingine ingawa nitategemea kuwa washauri wao wa ndani watahusika sana. Kwa mfano, kampuni ya kigeni ikimshitaki katibu wa Bunge au Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa kukiuka mkataba, AG ndie atakaewatetea. Ila usiniamini sana kwa vile mimi sio mwanasheria, mimi ni technician tu.

Amandla....
 
Wewe umesema dola ina mihimli mitatu. So state inaweza kuwa na branches?
Mkuu acha ukilaza,state ndiyo dola kwa lungha nyingine na ndo nchi au jamhuri.State/dola/nchi/jamhuri ya Tanzania ndo yenye mihimili mitatu kwa mujibu wa katiba ya nchi hii ya mwaka 1977 ambayo ni serikali,mahakama na Bunge.Kama hadi hapa hujaelewa naomba umtafute Oni sigara akufundishe kiswahili
 
Back
Top Bottom