Fatma Likwata ni moja ya tatizo

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nimekuwa nikifuatilia sana taarifa zake katika mpira wa miguu,ila nimegundua jambo moja.Ana mapenzi ya wazi wazi na club ya Yanga,jambo ambalo humfanya awe na utangazaji unaoelemea upande mmoja.Mfano akichukua maoni ya washabiki,inapokuwa ni dhidi ya simba,huchukua maoni yenye hisia hasi tu kama vile wapinzani wameonewa n.k bila ushahidi wowote.Yanga inapocheza,hata kama itaonekama wamebebwa namna gani,hutasikia akichukua maoni hasi dhidi ya Yanga.Ila kwa Simba ni kawaida.
Sikufahamu we Dada ila ukifanya kazi hiyo usipende kuwa mchochezi.Tunachukia washabiki.
Leo katika mechi ya mtibwa,umerudia yale yale.Unataka kuwaaminisha watu Simba hakustahili kushinda isipokuwa amebebwa!Hii ni kwa mujibu wa shabiki uliyempa muda bila kufikiri anajua kiasi gani kutafsiri sheria.
Acha hizo,mpira siyo taarab au bongo fleva
 
Mashabiki wa simba mna ugonjwa gani? Maana kila siku hamuishi kulialia mkiwalaumu watangazaji/waandishi wa habari kwa malalamiko yaliyojaa hisia ya kuisifia Yanga na kuisema simba! huku mkiwa hamna ushahidi wowote wenye mashiko!

Ni lini mtatoka kwenye minyororo ya mwenyekiti wenu mstaafu Ismail Aden Rage, aliyewaita mbumbumbu? Kwa sasa mnaongoza ligi kwa ushindi wa 100% huku yanga ikuanza kwa kichapo! lakini mashabiki wa yanga tumetulia kimya tu, hata mchecheto hatuna!
 
Nafikiri ungekutana na wenzio usiku huu kambini ili mtafakari jinsi ya kuifunga Zesco.
 
Mashabiki was Simba wana gubu kama mawifi.
 
Kwa hiyo siku zote akiwa studio huwa anatangaza habari tu za Yanga ?
 
Fatma ni mtangazaji,anaowahoji sio yeye anayewatafuta.
 
Naomba picha yake mabaharia kutoka mikoani tumshughulikiee.
 
Vyura FC msimu mzima walikuwa wakiwashwa washwa mara Ohh TFF, mara Ohh Marefa, mara Ohh Simba SC, na juzi mmeanza kulia kuhusu ratiba..!

Tunawaambia back to back itaendelea tu..SimbaNguvuMoja
 

Isije ikawa una chuki naye nje ya masuala ya mpira tehtehtehtehtehteh...Utuambie ukweli Ndugu kuhusu huyo dada...mmekorofishana kuhusu nini????
 
Ndo nani?
 
wanayofanya akina shafidauda, luambano, issa maeda na wengineo kutukanatukana na kukashifu YANGA wewe huyaoni, watu wa simba ni watata sana! !!
 
Watu wa Yanga tukiacha ushabiki wa mpira,je mnamiliki na bendi ya taarab?Maana comments zimejaa mipasho tupu.
Poleni kwa matokeo ya Leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…