Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Ukizungumzia waimba taarabu wa kike wenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni basi Fatma Mahmoud Nyoro maarufu kama Fatma Mcharuko ni namba one.
Waimba taarabu wengi wanapata shida kugandamizia/ kuimba nyimbo alizoimba Fatma kutokana na upekee wa sauti yake.
Wasanii wa jahazi modern taarabu walikuwa wanapata tabu sana kuimba nyimbo za Fatma kipindi kile Fatma mjamzito ,walikuwa wanaziharibu haswa tofauti na nyimbo za wengine hata wasipokuwepo lazima mbadala atakuwepo kuweza kuziba pengo hilo.
Bendi nyingi sana za taarabu zinatamani sana kuwa na Fatma katika bendi yao kutokana na upekee wa sauti.
Fatma alishawahi kutamba na vibao kama vile Mfamaji, Maruperupe,Aso kasoro, kwa sasa anasumbua na ngoma ya Siwaguni wala siwakohoi.
Fatma kwa sasa anaitumikia bendi ya Yah TMK na ndiye msanii aliyefanikiwa kuwajazia mashabiki bendi hiyo kutokana na umahiri wa uimbaji wake.