Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23]Ukitumia mfano wa malaika na usisahau kumsema ni malaika gani,maana yupo malaika mtoa roho,sauti yake sasa dah.
Hebu weka wibo wake mmoja tuusikie halafu weka na wimbo ulioimbwa na Malaika tuweze kufananisha.Ukizungumzia waimba taarabu wa kike wenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni basi Fatma Mahmoud Nyoro maarufu kama Fatma Mcharuko ni namba one.
Waimba taarabu wengi wanapata shida kugandamizia/ kuimba nyimbo alizoimba Fatma kutokana na upekee wa sauti yake.
Wasanii wa jahazi modern taarabu walikuwa wanapata tabu sana kuimba nyimbo za Fatma kipindi kile Fatma mjamzito ,walikuwa wanaziharibu haswa tofauti na nyimbo za wengine hata wasipokuwepo lazima mbadala atakuwepo kuweza kuziba pengo hilo.
Bendi nyingi sana za taarabu zinatamani sana kuwa na Fatma katika bendi yao kutokana na upekee wa sauti.
Fatma alishawahi kutamba na vibao kama vile Mfamaji, Maruperupe,Aso kasoro, kwa sasa anasumbua na ngoma ya Siwaguni wala siwakohoi.
Fatma kwa sasa anaitumikia bendi ya Yah TMK na ndiye msanii aliyefanikiwa kuwajazia mashabiki bendi hiyo kutokana na umahiri wa uimbaji wake.View attachment 1195219
NyororooNyoro sio tusi?