Fatuma Karume: Zanzibar inaidai Tanzania bara 4.6 trillion

Kama makubaliano yanasema wapewe 4% basi wapewe. Hakuna kuleta longolongo.

Wazanzibar wanaweza kuweka umeme wa Solar na Upepo ukawatosha, TANESCO kupeleka umeme huko ni kulea uchumba wa muungano tu lakini Wazenji wanavyo vyanzo vizuri vya umeme unaowatosha maana ni nchi ndogo
 
Huu ndiyo ukweli wenyewe mchungu. Zanzibar ni nchi mojawapo iliyo sehemu ya nchi mbili huru ziundazo JMT. Kwa hiyo stahiki zake zote zitokanazo na mambo yaliyoanishwa ndani ya muungano ni halali yake.
Nchi mojawapo umesema, nyingine ni ipi? Iko wapi?
 
Tuna siku kama 60 nyuma, hapakuwa na mtu anaomngelea sjui muungano, sjui deni la muungano, sijui umeenda ikafika wapi, mambo yalikuwa poa Kweli,

Mbona ghafula mambo yamekuwa mengi hivi?? JPM pengooo...,siyo pengo?
 
Kama makubaliano yanasema wapewe 4% basi wapewe. Hakuna kuleta longolongo.

Wazanzibar wanaweza kuweka umeme wa Solar na Upepo, TANESCO kupeleka umeme huko ni kulea uchumba wa muungano tu lakini Wazenji wanavyo vyanzo vizuri vya umeme unaowatosha
Wameweka majenereta yanawashinda kuendesha, waya ulipancha kule bahari, nini kilitokea?

Solar? Hauwezi kuwa uko siriasi, upepo? Wataweza ku-mantain quality ya umeme kwa kutumia vyanzo hivyo? Sisi pamoja na Hydro na Thermal, bado quality imetushinda.
 
Wameweka majenereta yanawashinda kuendesha, waya ulipancha kule bahari, nini kilitokea?

Solar? Hauwezi kuwa uko siriasi, upepo? Wataweza ku-mantain quality ya umeme kwa kutumia vyanzo hivyo? Sisi pamoja na Hydro na Thermal, bado quality imetushinda.
Sasa kwani hujui Zanzibar iliendelea mapema kabla ya bara?

Waachie nchi yao uone kama hawajageuka kitovu cha biashara East Africa
 
Isingekuwa mambo ya usalama hao Zenji tungewatema tu, kila siku wao kelele tu hizo 4.6 Trilioni anaona rahisi tu kuzitamka. Ameshindwa kuona ni kwa namna gani Zenji inavyonufaika zaidi na huu muungano kuliko Tanganyika kuanzia ardhi, kazi tukiwarudisha wote huko si kisiwa hicho kitazama na haya mabadiliko ya tabia nchi maana maji ya bahari yanazidi kuongezeka tu
 
HAYA YOTE NI MACHUKI AMBAYO MAFEDHULI TENA BILA AIBU YANAJARIBU KUMTETERESHA RAIS WETU KISAIKOLOJIA ILI AINGIE MKENGE NAJUA MAMA NI MWEREVU SANA ATAFAULU VITA HIVI NAANA VINAPIGWA KILA UPANDE ZANZIBAR NAFAHAMU WANA HAKI ZAO ZA KIKATIBA SIO VIBAYA ZIKALIPWA HATA KWA NJIA YA KIDOGO KIDOGO HAKUNA UBAYA WOWOTE LAKINI MAFEDHULI KAMWE HAMTAWEZA KUFANIKIWA, #SAMIA SULUHU HASSAN 2021-2030.
 
Dawa ya deni ni kulipa, kama ni kweli hayo makubaliano yapo
 
Sasa kwani hujui Zanzibar iliendelea mapema kabla ya bara?

Waachie nchi yao uone kama hawajageuka kitovu cha biashara East Africa
Halafu wakarudije nyuma? Hivi Comoro si ni visiwa?

Kwa bidhaa za magendo?

Ukumbuke hata ardhi ya kuwatosha wenyewe hawana, watatoka kwetu wataenda kwa wengine kuwa sehemu ya nchi na mshirika wa muungano.

Kilwa ilikuwa na umeme na sarafu, ikiwa yakwanza kwa huku bara giza kama nilisikia vizuri.
 
Kwani wameshalipa umeme wa Tanesco unaoenda huko? Kama vp kila mtu abaki kwake tu....yaani kimkoa tu kipewe asilimia 4%.....??
Zanzibar = 4,000,000/60,000,000 = 0.0333 = 3.3%. Nadhani ni sahihi wao kupata 4% ya misaada na mikopo, lakini mikopo ni lazima walipie kwa kiasi hichohicho cha 4%.
 
Usalama gani ?hii hoja ni dhaifu sanaaaaaaa ukweli ni kwamba Zanzibar inahitajika sana katika muungano ndio maana Mwalimu Nyerere alikuwa tayari Kuzika nchi yake ya Tanganyika kwa ajili ya muungano
 
Hakuna Muungano wa nchi mbili kuwa nchi mbili. Hapa tunadanganyana tu,kama kuna kero mama kwenye huu Muungano ni either kila nchi kivyake au tuwe nchi moja sasa wenye mamlaka wanapata kigugumizi kuamua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…