The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) limesema limepata ushahidi mpya kuhusu mauaji ya aliyekuwa Rais wa Marekani, John F. Kennedy, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Donald Trump.
FBI imesema imepata nyaraka mpya 2,400 zinazohusiana na ushahidi wa mauaji hayo, na tayari imeanza kuzifanyia kazi nyaraka zote.
Tamko la FBI linakuja siku chache baada ya Trump kuagiza kuwa upelelezi wa tukio la mauaji ya Rais Kennedy uanze upya, pamoja na mauaji ya mdogo wake, Robert Kennedy, na uchunguzi wa haki za kiraia za Martin Luther King Jr.
Mauaji ya Rais Kennedy yaliyotokea Novemba 22, 1963, huko Dallas, Texas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey Oswald, yamekuwa yakihusishwa na nadharia nyingi kwa miaka mingi, huku mamilioni ya Wamarekani wakiwa na mashaka juu ya wahusika halisi wa mauaji hayo.
Mwaka 2023, katika kura za Gallup, asilimia 65 ya Wamarekani walionyesha kutoamini ripoti ya Tume ya Warren, ambayo ilihitimisha kwamba Lee Harvey Oswald alimua Rais Kennedy bila kushirikiana na mtu yeyote.
Pia Soma:
www.jamiiforums.com

Pandora Box:Trump anafungua ya JFK na MLK US huku TZ tunasubiri ya JPM,JK na SSH kubaka Katiba ya CCM na JMT je,Mungu kampa TAL kazi hiyo maalum?
..waliopindua si CCM wenyewe? ..wana-CCM ambao hawajaridhika ndio wanaopaswa kuchukua hatua. ..waige mfano wa Chadema ambao hawakuridhika na mambo fulani ktk chama chao wakaamua kuchukua hatua. Ahahahah