FBI yaonya uwezekano wa Iran kufanya shambulio Marekani

FBI yaonya uwezekano wa Iran kufanya shambulio Marekani

In The US kuna wengi wanasema wanataka kujifanyia wenyewe ili kuwe na justifications za kuweka boots on the ground huko Iran, mpango ni kwamba zirushwe kutokea Mexico then waseme ni collaboration kati ya Iranian regime na Mexican Mafia gangs ili wawashe moto wa kinomanoma huko.
Kama yale ya Sept'11th baadhi wanavyodai iliwa crafted na wao wenyewe.
Bila ile sept 11 huenda hadi leo wasingekuwa wanaendesha biashara ya mafuta huko uarabuni.
US ina reserve ya mafuta kwa takribani miaka 100.
 
Bila ile sept 11 huenda hadi leo wasingekuwa wanaendesha biashara ya mafuta huko uarabuni.
US ina reserve ya mafuta kwa takribani miaka 100.
Focus, control, mastery with being ahead of the curve.
💪🏾💪🏾💪🏾💪🏾
 
Nimekuelewa ila umenielewa nilichokwambia kwamba nini atakipa Iran km akithubutu kutuma hizo drones kwenye ardhi ya U.S? Ingawa kimkakati hawezi hapo maelezo yamejitosheleza kabisa kabla hayarusha hizo drones atapokea kisago kitakatifu iwe funzo kwa wengine wenye tabia km za kwake, mimi sifurahii kinachotokea ila sifurahishwi na Iran pia maana anajijua ana uwezo mdogo ila anajitafutia matatizo yeye na dunia kwa ujumla, U.S hapigani vita ya hasara siku zote anatarget faida hii vita ina faida kubwa kwa U.S kuliko Iran, Iran anapata hasara mara dufu kuliko U.S pamoja na kiburi chake japokua anaona km U.S anapoteza ila sio hivyo anatuma drones nyingi za USD 20,000 ambazo zinatunguliwa kwa kombora la USD 2 Million haina maana U.S anaingia hasara km anavyofikiri
Kwa maelezo yako ni kama Iran ndio kaanza kushambulia. Wewe ulitaka vipi apigwe akae kimya au? sasa nani kila siku yuko kwenye press kupiga kelele. Huyo Trump wenzake tu hawajui anataka nini. Hivi vitisho havina faida nimekwambia Newyork ilipigwa na walifanya nini Afghanstan? mwisho wa siku walikimbia wenyewe Taliban anatawala. Tutajie vita yoyote USA kama yeye alishinda peke yake. Watu hawaogopi vitisho atapiga nini raia au? Unasema hapati hasara anaokota hayo mabomu.
Twende taratibu

Emu tulia kwenye kiti kisha soma

Katika vita yoyote, hasara huwa ni ya pande zote mbili, lakini aina ya hasara hutofautiana kulingana na nguvu ya kijeshi na hali ya kiuchumi ya kila nchi. Kulingana na hali ya sasa (Machi 2026), huu hapa ni uchambuzi wa nani anapoteza nini:
1. Hasara kwa Upande wa Iran (Hasara ya Moja kwa Moja na ya Kimfumo)
Iran ndiyo inayobeba mzigo mkubwa zaidi wa uharibifu wa ndani na kijamii kutokana na mashambulizi yanayofanyika katika ardhi yake.
* Viongozi na Miundombinu: Mashambulizi ya hivi karibuni (Februari/Machi 2026) yamesababisha vifo vya viongozi wakuu, akiwemo Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei. Pia, miundombinu ya nyuklia na kijeshi imeharibiwa vibaya.
* Vifo vya Watu: Idadi ya vifo nchini Iran ni kubwa zaidi, ikikadiria zaidi ya watu 1,200 waliouawa na maelfu kujeruhiwa, huku mamilioni ya raia wakihama makazi yao.
* Uchumi wa Ndani: Kufungwa kwa Mlango-bahari wa Hormuz kumepunguza uwezo wa Iran kuuza mafuta yake mwenyewe, jambo linalozidisha mfumuko wa bei na uhaba wa bidhaa muhimu nchini humo.
2. Hasara kwa Upande wa Marekani (Hasara ya Kiuchumi na Kimkakati)
Ingawa Marekani haishambuliwi moja kwa moja kwenye ardhi yake, inapata hasara kubwa ya fedha na ushawishi.
* Gharama za Vita: Pentagon inakadiria kuwa vita hii inagharimu Marekani kati ya Dola milioni 890 hadi bilioni 1 kwa siku. Katika siku sita za kwanza pekee, walitumia zaidi ya Dola bilioni 11.
* Uchumi wa Dunia: Bei ya mafuta imepanda hadi kufikia zaidi ya Dola 100 kwa pipa, jambo linalosababisha kupanda kwa gharama za maisha nchini Marekani na duniani kote. Soko la hisa la Marekani limekuwa likiyumba kutokana na hofu ya wawekezaji.
* Wanajeshi na Kambi: Wanajeshi wa Marekani walioko kwenye kambi za Mashariki ya Kati (kama Qatar, Bahrain, na Kuwait) wamekuwa shabaha ya makombora ya Iran, na kusababisha vifo na majeraha kwa askari kadhaa.
Muhtasari wa Hasara
| Aina ya Hasara | Iran | Marekani |
|---|---|---|
| Vifo/Majeruhi | Juu sana (Raia na Wanajeshi) | Chini (Wanajeshi pekee) |
| Miundombinu | Uharibifu mkubwa wa ndani | Uharibifu wa kambi za nje |
| Uchumi | Kuporomoka kwa mfumo wa ndani | Mfumuko wa bei na gharama kubwa za vita |
| Siasa | Hatari ya kupoteza utawala (Regime Change) | Shinikizo la kisiasa nyumbani kutokana na gharama |
Nani anapata hasara zaidi?
Kijeshi na kibinadamu, Iran inapata hasara kubwa zaidi kwa sababu vita inapiganwa ndani ya mipaka yake. Hata hivyo, kiuchumi na kimkakati, Marekani inapoteza utulivu wa soko la dunia na mabilioni ya dola ambayo yangeweza kutumika kwa maendeleo ya ndani.

Nadhani tunaelewana hapo.
Mimi sijawahi kukubali siasa za Iran hasa katika kuwa na vikundi nchi za watu na kuvipa support ila sijawahi kukubaliana na siasa za USA kwa uharibifu wao wanaofanya duniani. Hii ni moja ya mara chache kakosa uungwaji wa mkono hata kutoka kwa washirika wake wa karibu wote wamepiga pause. Katika vita hii hajafanikiwa hata lengo moja yeye alidhani hii kama Libya, akianguka mkubwa nchi inaanguka. Kumbuka yule sio alikuwa kiongozi wa kisiasa tu bali ni wa kidini pia kwa madhehebu ya Shi'a. Trump uwelewa wake mdogo sana yeye yupo kibiashara tu, kutwa akiongea mafuta ya Venezuela, kuongeza kodi kila kukicha kwa vitisho kwenye siasa zero, kazungukwa na watu YES BOSS, ukipingana naye tu mawazo wewe adui. wale wenye nguvu ndio marafiki zake. Kitu pekee namsifu kupiga chini wale mbwa wa LGBTQ siku hizi kimyaa. Democratic kilichowapotezea mvuto kuwa mlengo wa kushoto kupitiliza maana kila ukiamka haki za mashoga tu. Kwa hili Trump salute mengine yupo zero. Hataki kukosolewa yaani huyu angekuwa katika nchi zetu angekuwa bonge la Dictator.
 
Kama wamepata 15000 km missiles wasiwasi lazima uongezeke.
 
Back
Top Bottom