Kifupi ni wapuuzi kupita hawa jamaa, Mimi nimeamua hadi kuifuta App yao ya "Barcelona Live". Kila siku tetesi, nafikiri wana mpango wa kuiua na kuiteketeza timu pamoja na Academy ya Lamasia.
Haingii akilini, Dembele, Jean Michael Seri na timu zao zimeshakubali kuwaachia, lakini uongozi wa Barca kutwa nzima wanajizungusha tu yaani hawataki kutoa pesa ili kukamilisha usajili huo.
Hapo hapo unakuta wana ng'ang'ana Mara cjui Coutihno Mara Angle Dimaria wakati timu zao zimeshasema hawaondoki hawa, mfano kama Coutihno ni wazi kuwa hawezi ondoka kwa 7bu ktk mkataba wake kuna kipengele hakimruhusu kwenda popote msimu huu.
Yaani hapa, Messi akisepa kwenda Man City ntafurahi sana kwani itakuwa fundisho kwa uongozi. Uongozi gani huo hauna future na team na maendeleo endelevu ya sasa?
Kuna wachezaji wazuri sana vilabu vyao vilikuwa vimeshakubali wajiunge na Barca, mfano ni Jean Michael Seri na Martinez lakini cha kushangaza wameachwa na badala yake eti wakamsajili mzee, Paulihno miaka 29 wakazi gani huyo ameshazeeka tayari.
Nasikitika sana kwanini timu inakufa hivi hivi tena kwa klabu kubwa na tajiri kama Barcelona wakati wachezaji wazuri wamejaa kote duniani.
Aibu ya mwaka hii....
Sent using
Jamii Forums mobile app