FC Genk yakataa dau la Euro milioni 13 kwa Mbwana Samatta kutoka Cardiff City ya Uingereza

FC Genk yakataa dau la Euro milioni 13 kwa Mbwana Samatta kutoka Cardiff City ya Uingereza

Uzuri wa Epl atazidi kujitangaza, na cardiff wana matatizo sana kwenye 'striking force' yao, bila shaka angekua na namba ya uhakika kama angeenda. Timu pekee ambayo ina asilimia kubwa ya kushuka so far ni huddlesfield, mpaka mtaalamu big Sam mwenyewe kaikataa[emoji2]

the Legend☆
 
Hamna madogo wengine wanaochipukia, kitengo ndiyo kinajukumu la kutengeneza Ma Samatta wengi Tanzania ila wamebaki tu kuratibu mipango ya ccm kubaki madarakani
Wewe unafanya nini kutengeneza samata wengine au ndio unapiga kelele tu?
 
Updates: Cardiff City wamsajili Oumar Niasse kwa mkopo kutoka Everton.

1547675663101.png

Oumar Niasse

Timu ya Cardiff City imemsajili kwa mkopo mshambuliaji mwingine aitwae Oumar Niasse kutoka klabu ya Everton.

Hivyo inaonekana timu hiyo imeamua kufanya usajili wa mkopo na kuachana na kuwasajili Emiliano Sala na Mbwana Samatta.

Niasse ambae pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal, alisajiliwa na Everton kutoka timu ya Lokomotiv Moscow msimu ulopita na msimu huu haijawahi kucheza mechi hata moja kwa timu yake hiyo ya Everton.

Meneja wa zamani wa Everton Roberton Martines alimsajili Niasse kwa pauni milioni 13.5 mwaka 2016 na tangu wakti huo mchezaji huyo amekuwa akikaa bench.
 
Wamwache aende mbona mpunga mzuri sana huo? Wamesema dau lao ni kiasi gani?

Klabu ya Genk ya Ubelgiji imekataa dau la Euro milioni 13 kutoka kwa timu ya Cardiff City ya Wales.

Dau hilo ambalo liliwekwa jana jioni lilikuwa ni la kwanza kufanywa na haijulikani kama Cardiff City wataongeza dau hilo.

Cardiff City wanatafuta mshambuliaji na pia wanamfuatilia mshambuliaji wa Nantes Emiliano Sala.

Habari zaidi kufuata.

NB:
Habari hizi ni kutoka vyanzo mbalimbali.
 
Wamwache aende mbona mpunga mzuri sana huo? Wamesema dau lao ni kiasi gani?

Cardiff walifanya kitu chaitwa "registration of interest" kwa Mbwana Samatta lakini Genk wakakataa mara moja kwani dau lilikuwa ni hilo la 13 Mil Euros.

Lakini mpaka sasa timu ya Schalke nayo imefanya hiyo registration of interest na Genk wanafikiria.

Timu ingine ambayo jioni hii imefanya hivyo ni Southampton ya Uingereza ambayo inapigania kubaki kwenye PL.

Ila kuna uwezekano mkubwa Samatta akaenda Schalke au akabakia Genk.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
EPL itakuwa bomba zaidi kwa maoni yangu.

Cardiff walifanya kitu chaitwa "registration of interest" kwa Mbwana Samatta lakini Genk wakakataa mara moja kwani dau lilikuwa ni hilo la 13 Mil Euros.

Lakini mpaka sasa timu ya Schalke nayo imefanya hiyo registration of interest na Genk wanafikiria.

Timu ingine ambayo jioni hii imefanya hivyo ni Southampton ya Uingereza ambayo inapigania kubaki kwenye PL.

Ila kuna uwezekano mkubwa Samatta akaenda Schalke au akabakia Genk.
 
Nafikiria porojo zenu zitakua zimeisha. Cardiff wameshasaini kifaa cha Kiargentina ambae ameshatupia zaidi ya goli 10 katika ligi ya ufaransa msimu huu.
 
Back
Top Bottom