FCC mmebariki uhuni, wizi na utapeli wa makampuni ya simu?

FCC mmebariki uhuni, wizi na utapeli wa makampuni ya simu?

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Haya majitu ni matapeli na majizi yasiyo na aibu wala huruma, kwa bahati mbaya pale pia watu.vyombo vilivyotakiwa kuwasaidia WANUKA JASHO wa nchi hii wal hawana habari kabisa

Wamekaa meza kuu na majizi hayo wanakula na kusaza , wanukajasho watatjijua wenyewe

Miaka 3 /4 iliyopita hata 2 iliyopita ilikuw abei ikibadilika unakuta ni kampuni moja au mbili wanuka jasho wanakuwa na alternatives ya kukimbilia kampuni nyingine, mafano hai ni Halotel walijipatia wateja wengi sana ila kwa sasa ndani ya siku mbili unakuta wanapandisha kwa pamoja na kwa viwango vinavyofana kabisa.

FCC tume ya ushindani ina maana hamlioni hili jamani? Agh.

HUU NI UMAFIA LA COSA NOSTRA STYLE, HII NI CARTEL WANAKAA MEZANI KWA PAMOJA NA VICHEKO JUU YAKE WAKIJUA WANUKA JASHO HAWANA PA KUKIMBILIA WATAONGEA WATAUFYATA NA HAPO WAZIRI ANAKUWA KESHAWAPASHA VYA KUTOSHA
 
Data Tanzania wanaiba aisee yaani hapo Malawi 4 GB wanauza kwa wiki kama Tsh 2000 tuu harafu haiishi hata uangalie vitu live kwa muda mrefu ila Bongo walivyo majambazi sekunde chache tuu unanunua ya ten harafu wanakupa 75% ya matumizi yako data ni sehemu rahisi ya kuibiwa watu na wahusika wapo kimya...
 
Wajinga sana hawa majitu,miezi miwili iliyopita nilikuwa na kifurushi cha 3000tsh unapata dk 250 na 1gb,wakakipunguza kikawa tsh 2000 ni dk 150 na 1gb,ndani ya mwezi huo wakapunguza tena kwenye hio tsh 2000 ikawa ni dk 80 sms 20 na 1gb nimeendelea nacho leo hii nataka kununua muda wa maongezi hata mwezi haujaisha tsh2000 nakuta wamepunguza tena eti ni ile buku 2000 unapata dk 30 sms 30 na 1gb,hivi kweli hii sawa,soon nawahama hawa @HALOTEL sitaki tena mazoea nao nahamia TTCL
 
Back
Top Bottom