BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, iliyofanyika leo Mei 21, 2024, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge, amesema kiasi hicho cha fedha kimeongeza chachu ya ushiriano wa pamoja wa kukuza maendeleo ya jamii kupitia Wiki ya AZAKi.
Rutenge amesema kuwa ili kuweza kusonga mbele sauti mbalimbali za wadau na wabia zinahitaji katika kuchochea mchakato wa maendeleo.
“Ili tuweze kusonga mbele na kuiona Tanzania tunayoitaka, sauti za wadau na wabia mbalimbali zinahitajika kusikika na ziwe sehemu ya kutoa mchango katika mchakato mzima wa maendeleo ambayo yatasaidia kujenga maono ya kulipeleka Taifa letu mbele” amesema Rutenge.
“Ushirikiano huu utasaidia kubadilishana uzoefu, Vodacom Foundation watanufaika na uzoefu tulionao katika kusimamia miradi ya maendeleo, kuchochea usawa wa makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wanawake, vijana, watoto na watu wenye ulemavu. FCS nao watanufaika katika kuunganisha watu kwa kutumia teknolojia kwa kuzingatia nchi ipo kwenye mapunduzi ya teknolojia,” ameeleza Rutenge.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Foundation Tanzania, Zuweina Farah, amesema ili kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, ushirikiano wa pamoja unahitajika kati ya AZAKi, Sekta Binafsi na Serikali.
Pia ameongeza kuwa, lengo la Vodacom Foundation Tanzania ni kukuza ushirikiano katika kuleta maendeleo ya jamii, kuimarisha utawala bora na kuboresha mazingira ya Biashara nchini.
Wiki ya AZAKi mwaka huu imebebwa na kauli mbiu ya isemaho ‘Sauti, maono na thamani’ ambayo inaambatana na lengo Kuu la FCS la kuwezesha maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.