Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dr. Dau Kuikoa Bandari?
Members, nimeona hiyo habari kwenye kijarida cha Cheche kwamba Dau kuiokoa bandari kama atateuliwa kuwa mkurugenzi wa bandari. Lolote linaweza kutokea, lakini mimi niko kwenye upande wa kushindwa kwa Dau kuikoa bandari kwa sababu moja tu ya kimsingi. Wengi wa wakurugenzi wa mashirika ya hifadhi ya mifuko ya jamii na pensheni wanafanya vizuri sana na wanasifiwa. Kwanini??? kwa sababu wana nguvu ya kisheria ya kukusanya na kupata mapato. Mishahara ya wafanyakazi inakatwa from the source na kupelekwa kwenye mashirika haya. Kwahiyo mkurugunzi na menejiment yako unafanya kazi ya kupanga utumie vipi hizo fedha. Hawawekezi kwenye mtaji. kwahiyo capex iko chini na hata opex. Mataka alikuwa NSSF na alifanya vizuri, kapelekwa ATCL kaisindikiza kaburini. Ni kwa sababu kapewa field ambayo haijui na inahitaji nguvu za ziada kuvutia wateja, kuwafurahisha na kulipa gharama za uendeshaji. NSSF, PPF, LAPF, PSPF etc tofauti ya kulipa gharama za mishahara na kodi ya pango wana gharama gani zingine. ndio maana wanajenga majengo kila mahali nchini, wanawakeza kwenye hisa na wanatoa mikopo, mwisho wa mwezi wanawakoromea waajiri na kuvuta cheque zao. Sasa kuna uwezekano mkubwa kwamba Dau akaipeleka bandari kaburini kama alivyofanya Mataka na ATCL. cha msingi siyo kupima uwezo wa Dau kuwa mkurugenzi wa NSSF na kuifanya NSSF ifike mahali hapo ilipo bali uwezo wa mtu mwenye upeo na uelewa wa biashara ya bandari. Na isije kuwa tunapima mafanikio ya NSSF kwa kuona maghorofa yanayojengwa wakati akiba za wafanyakazi hazizai riba, matibabu ni hospital za hovyo, gharama za mazishi kiduchu, gharama za kujifungua mpaka mzazi azisotee then tunasema Dau kafanya vizuri. Kuna tetesi shirika lime overspend kwenye miradi ya chuo kikuu cha dodoma na iradi mingine ambayo imeanzishwa kisiasa na sasa Dau anataka kutoroka. Mwenye data atusaidie. Bandari ina skills zake za kui run. mie sioni sababu kwanini nafasi ya mkurugenzi wa bandari isitangazwe watu waka apply interviews zikafanyika na reputable firms in the world kabla hajapewa nafasi hiyo. Sitasikitika akipewa mgeni with a condition kwamba ata train watanzania watano as successors within five years. Sasa hii mambo ya kwamba alifanya vizuri NSSF ndo atafanya vizuri bandari ni balaa! kuna mifano ya mawaziri ambao walikuwa wazuri kwenye wizara fulani na walipopelekwa wizara nyingine walichemsha kiasi cha kuwa cost uwaziri wao.
Naomba kutoa hoja.
Mods walinitumia alert kwamba nimekuwa kimya hata swali siulizi! Nikahisi karibia nifutwe uanachama wa the home of great thinkers club. At least by now niko active na naweza kukaa kimya tena
Hivi ni kweli kwamba Dr. Dau ana udini wa msimamo mkali? Kama kweli hii inawezaje kuingilia utendaji wake?