Jamani hebu tuache uzushi! Ukiangalia noti zetu zote haziko kwenye kipimo kimoja yaani angalia ukubwa wa noti ya shilingi 1000, ya 2000, ya 5000 na 10,000 zote zinatofautiana lakini zote zinatolewa na mashine hiyo moja. Hebu tuambie ni wapi ulienda ukakuta kila noti inatolewa na mashine tofauti tofauti? Wana-JF hivi kweli tunakazana kuwalaumu BOT kwa ajili ya thread ya kizushi kama hiyo? Au kuna mtu gani hajawahi kuchukua shilingi 1,000 au 2,000 kwenye ATM? Mimi sitaki kuamini kwamba safari hii BOT wametengeneza noti ndogo kama stemp (hapo litakuwa jambo jingine litakalohitaji maelezo ya kina)!!
Na suala la kubadili noti safari hii mimi sioni kama ni jambo la uzembe! Nawaunga mkono kwa asilimia zote, hivi hatuoni ajabu kuendelea kutumia noti zenye saini za watu kama akina B.P. Mramba na D. Balali? Watu wanaweza kuuliza sasa tutakuwa tunatengeneza noti kila tunapobadili magavana na mawaziri wa fedha? Labda huu ndo uwe mjadala wa kuona nini kifanyike ili kuzuia hali hiyo isiendelee kutokea. Pengine tunaweza kuwa na Saini ya mtu mmoja maalum (sema kama vile Mwl. Nyerere) ambaye hata akifa iendelee kuwepo kwenye noti zetu na hili linapaswa kuzungumzwa kwenye Katiba yetu mpya ili kuzuia utengenezaji holela wa fedha zetu. Hivyo wana-JF nasema tena naunga mkono wazo hili la kubadili noti ili tusiendelee kuona saini za akina Mramba na Balali (Zinatuchefua bure).
Wazo la nani agharamie hayo marekebisho ya ATMs (kama kweli kuna haja ya kurekebisha), hiyo itakuwa gharama ya mwenye biashara na wala hauwezi ukawa mzigo wa BOT. Ni wewe mwenyewe ndo unataka biashara yako iende vizuri na kwa ufanisi hivyo lazima uingie gharama. Endapo watatudanganya kwamba BOT imegharamia marekebisho hayo tutajua ni aina nyingine ya ufisadi!!!!!!