CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,858
- 687
WanaJF wenzangu
Jaribu kumuuliza kijana wa sasa umri wa 20 hadi 35 bima yake ktk mapenzi ni nini?? Atawezaje kujiamini na kujihakikishia kuwa mpenzi aliyenaye hatamuacha???
Nane kati ya vijana kumi watakwambia kuwa "bima" ni kuwa na uwezo wa kumudu mazingira ya maisha ya kisasa, kuwa na gari, kazi nzuri na sometimes hata nyumba yenye hadhi, kinyume na hapo hakuna "kinga" ya mapenzi.
Inawezekana jambo hilo ni kweli, imeshawahi kutokea mara kadhaa mpenzi wa muuza mitumba pale Manzese Big Brother amechukuliwa na "kula kulala" mmoja wa Mikocheni eti tu kwa sababu tu "kula kulala" anaendesha gari la nyumbani kwao na anapesa kiasi za kutoka nae. Achana na hilo, pia inaweza kutokea kwamba mpenzi wa "kula kulala" kama huyo amechukuliwa na "*****" mmoja ambaye kutokana na "upambe" wake kwa watu maarufu wa mjini pesa mbili tatu hazimpigi chenga na hubadili "magari ya watu" kila mara.
Katika hali kama hiyo mtu aliyeporwa au kuchukuliwa mpenzi wake hujihisi ana mapungufu na pengine mawazo yake yakamfanya ahisi kwa vile hana gari au pesa za kutosha basi nafasi yake ktk mapenzi haina uhai kama mdudu mbu!! Ajabu!!!
Hii ni imani ya vijana wengi, wengi wanaamini kuwa uhalisia wa mapenzi ktk ulimwengu wa leo unakuja tu kwa mtu kujiweza kwa kila kitu, awe na pesa, gari, na pengine hata nyumba yenye hadhi ingawa itakuwa ya kupanga tu.
Lakin udadisi wangu juu ya mahusiano ya kimapenzi nimegundua kwamba watu wengi wanaowaacha wapenzi wao na kwenda kwa wapenzi wengine kwa sababu ya pesa au vitu vingine vya anasa, maisha yao ya kimapenzi huishia kwa mwisho mbaya sana. (Sijui Jaffarai anafit hapa??). Huishia kujuta kwa sababu mara zote wale wanaowaacha wapenzi wao wa kweli na kufuata watu wenye uwezo na vishawishi vya vitu kama magari, pesa na muonekano wa kimwili hawapati mapenzi ya kweli mara nyingi huachwa ktk muda mfupi sana.
Matokeo yake watu wa aina hii hujuta na kutaka kurejea kwa wapenzi wao wa zamani lakin bahati mbaya kwao hukuta zile nafasi walizoziacha zimeshajazwa na watu wengine wenye mapenzi ya kweli. Ni wachache sana wanaobahatika kupata nafasi ya pili, na hata hivyo nafasi hiyo hutolewa "kimachale" kwa sababu aliyeachwa mara ya kwanzahana imani tena na mwenzie. Ubaya wa kuachwa au kuingia kwenye mapenzi ya aina hii ni kwamba taratibu mwanamke au mwanaume mwenye kushawishika kirahisi hujikuta akiishi kwenye mapenzi yasiyo na msimamo na hapa ndipo anabatizwa majina kama "kicheche" na mengineyo
Katika hali halisi mapenzi ya kweli hayaguswi wala wala kushawishiwa na vitu vya kuvutia bali yanajengwa na udhati wa hisia za mtu mmoja kwa mwingine bila kujali uwezo wa kukabili majukumu ya kawaida ya kimaisha.

Samahanini sana kwa maelezo marefu, lakin nimelazimika kuyaandika hivi kama mchango wangu wa kuelimishana na kurudisha hadhi ya MMU iliyopotea.
CPU