Katika Watanzania wanaoziharibu (Fedha za Noti) za Tanzania ni makondakta & madereva wetu wa vyombo vya moto yaani magari ya abiria na mizigo wakishirikiana na wasimamizi wa Sheria za nchi hii (Traffic).
Fedha tajwa hapo juu hutolewa kwa njia ya kidhalilishaji kwa sarafu zetu na askari pia. Noti hizo hukunjwa na kufinyangwa kiasi kwamba unakuwa ni uharibifu wa sarafu ya nchi. Je, sheria zinasemaje kuhusu hili? Ni halali kwa askari wenye ajira/ujira halali kukusanya fedha za Ku brush viatu bila kutoa risiti? Noti nyingi za Tshs zenye thamani ya elfu moja, mbili na tano zinahusika na madhara haya. Wizara ya fedha haifahamu hili?
Hadhi ya Utumishi wa Umma inadhalilika huku Kila mmoja akijifanya haoni? Hii siyo rushwa?
Kwenye baadhi ya miji hapa nchini wamiliki/waendesha vyombo vya moto wanachangishana na kuwasilisha kiasi fulani cha fedha kwa siku,wiki ama mwezi kwa hao maofisa katika maeneo hayo. TAKUKURU badala ya kuchunguza hayo, wataanza kuwasaka watoa taarifa/dondoo muhimu.
Kila mtu akijifanya haoni, hasikii na kujifanya mambo ni shwari tunajenga Taifa la aina gani? Tafsiri ya neno Rushwa huwa ni nini hasa?