SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 1,213
- 1,918
Pamoja na fedha ya Serikali kuwekewa Ulinzi mzito kwenye awamu hii ya tano lakini bado wapo wajanja wanaendelea na upigaji tena kiulaini.
Ipo hivi, huu mchezo unapigwa Halmashauri za Wilaya/Manispaa. Wakitaka kupiga hela wataanza kutoa Taarifa kwa wafanyakazi katika Wilaya husika kwamba kutafanyika Uhamisho wafanyakazi wa ndani ya wilaya yao, haswa haswa waalimu kutokana na uwingi na uoga wao huwa ndo wanaotumika. Baadae wataingiza fedha kwenye akaunti za wale waalimu wanaoonekana watafaa kwa huu mchezo wao. Au muda mwingine hawatoi taarifa za Uhamisho ila wataingiza hela kwenye akaunti tu.
Sasa baada ya siku mbili au tatu huyu mfanyakazi aliyeingiziwa fedha ya Uhamisho anapigiwa simu na mtu wa Halmashauri akimweleza kuwa amehamishiwa kwenda shule ya mbali halafu atamwambia kama anataka asipelekwe basi amrushie zile fedha zote za Uhamisho alizoingiziwa na atapangiwa shule ya karibu.
Kama kawaida mtu mfano tayari yupo anaishi na familia yake ukimletea habari za Uhamisho kwenda sehemu za porini basi atakuwa tayari kufanya lolote, kwahiyo atarusha zile pesa kwa yule aliyempigia naye atahamishiwa shule ya karibu ili kuhalalisha matumizi ya fungu la fedha.
Kwahiyo hawa akina CAG wakipita kila kitu kinakuwa sawa na wao maisha yanaendelea..
Nafikiri wazo la Kishimba lifanyiwe kazi hiko Chuo cha Wizi kianzishwe mapema.