Fedha za bima kwa wote kukatwa kwenye line za simu, mpango wenu Serikali ni Watanzania tuache kabisa kuwasiliana?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Kuna watu mpaka unafikiria mtu kama huyu kafikaje bungeni, maana ni zaidi ya weupe kichwani, watupu kabisa!

Kodi zote hizi mnazotuumiza nazo wananchi bado unataka ziongezwe nyingine kwenye line za simu?

Hii siyo ya kukalia kimya!

Dunia inapiga kasi kwenye digidali lakini Viongozi wetu ndio kwanza wapo mstari wa mbele kuturudisha nyuma!

Mbunge unajua hali za wananchi wako, gharama za maisha zinapanda kila kukicha, baada ya kutafuta njia ya kupunguza mzigo unataka umuongezee tena kodi?

Ndio mmeona hii ndio itakuwa njia rahisi ya kuwafanya watu wasipate taarifa, mpite bila kupingwa na kuendesha serikali kama vile mnaendesha ng'ombe?

Wale wa kukaa kimya na kuona matatizo yanawagusa watu fulani, hii inaenda kukugusa hata wewe! Piga kelele, embu tuache kuwa wajinga na kukubali upuuzi kama huu kuendelea kufanyika!

Raia wa Gairo, Mbunge wenu Ahmed Shabiby kapendekeza takataka huko bungeni, endeleeni kuwa chawa tuendelee kusaga meno mpaka kiama!

Kwa nafasi yako piga kelele, hata wewe unayetoa povu hapa unafanya kwa nafasi yako, usikae kimya wakati una uwezo wa kusema, kama Rais huwa anapita amini na wale wengine wanapita kuchungulia kama mmekubali au lah, huwezi kwenda kuandamana piga spana JF dawa iwaingie huko huko walipo!

====

Pia soma Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
 
Simu zenyewe mnatumia kutongozea na kutazamia ngono wazo la mbunge ni zuri usipoumwa wewe ndugu yako ataumwa.
Achen negativity wabongo, wangapi wanakufa kwa kukosa matibabu kisa mia Tano.
 
Makampuni ya Simu hayakuja Nchini kuwa Tehama ya Serikali kukusanyia Mapato yanatafuta Faida laa sivyo yataondoka na kuhamia Nchi zingine.
Yaende mbona yanaingiza faida nyingi kuliko
Mfano kwa sms kuna kampuni inakusanya bilioni moja kwa siku.
Sh 50 mara milioni 25 kwa siku.
 
K

Kwa hiyo mtoa pendekezo anapendekeza mteja ndiye akatwe hicho kiasi au shirika la mawasiliano ndilo likatwe hicho kiasi kwa kila mteja?
 
Tena mm naomba makato iwe 80%, yaani ukiweka buku wanachukua 800, ukiweka 500 wachukue 400 na ukiweka buku 5 wachukue buku 4.

Kwasabb mawadiliano mengi ya wabongo siyo yenye tija, yanahusu kudanga, umbea, na mijadala ya Simba na Yanga.
 
Wakuu,

Kuna watu mpaka unafikiria mtu kama huyu kafikaje bungeni, maana ni zaidi ya weupe kichwani, watupu kabisa!

Kodi zote hizi mnazotuumiza nazo wananchi bado unataka ziongezwe nyingine kwenye line za simu?

Hii siyo ya kukalia kimya!

Dunia inapiga kasi kwenye digidali lakini Viongozi wetu ndio kwanza wapo mstari wa mbele kuturudisha nyuma!

Mbunge unajua hali za wananchi wako, gharama za maisha zinapanda kila kukicha, baada ya kutafuta njia ya kupunguza mzigo unataka umuongezee tena kodi?

Ndio mmeona hii ndio itakuwa njia rahisi ya kuwafanya watu wasipate taarifa, mpite bila kupingwa na kuendesha serikali kama vile mnaendesha ng'ombe?

Wale wa kukaa kimya na kuona matatizo yanawagusa watu fulani, hii inaenda kukugusa hata wewe! Piga kelele, embu tuache kuwa wajinga na kukubali upuuzi kama huu kuendelea kufanyika!

Raia wa Gairo, Mbunge wenu Ahmed Shabiby kapendekeza takataka huko bungeni, endeleeni kuwa chawa tuendelee kusaga meno mpaka kiama!

Kwa nafasi yako piga kelele, hata wewe unayetoa povu hapa unafanya kwa nafasi yako, usikae kimya wakati una uwezo wa kusema, kama Rais huwa anapita amini na wale wengine wanapita kuchungulia kama mmekubali au lah, huwezi kwenda kuandamana piga spana JF dawa iwaingie huko huko walipo!

====

Pia soma Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
Umesikia kauli y serikali?
 
Tena mm naomba makato iwe 80%, yaani ukiweka buku wanachukua 800, ukiweka 500 wachukue 400 na ukiweka buku 5 wachukue buku 4.

Kwasabb mawadiliano mengi ya wabongo siyo yenye tija, yanahusu kudanga, umbea, na mijadala ya Simba na Yanga.
Fact
 
Back
Top Bottom