Fedha za dhamana zitolewazo mahakamani huwa zinaenda wapi?

Fedha za dhamana zitolewazo mahakamani huwa zinaenda wapi?

Naomba kuuliza, kama umemdhamini mtu mahakama ya Mwanzo amepangiwa tarehe ya kurudi Mahakamani, ikifika tareh husika kwani ni lazima mdhamini uwepo au yey mtuhumiwa akienda si basi inatosha?

Au??
mkuu hili swali lilikuwa nje ya uwezo wangu, ila nashukuru mchanguaji hapo juu ametoa ufafanuzi
 
Kuna zingine unaambiwa na baadhi ya wahudumu wa mahakamani unabei gani ili tukupe dhamana ya ndugu yako. Sanasana Mahakama za Mwanzo unafunguliwa droo unaambiwa weka humu kakae nje tutakuita. Hizo nazo zinaenda hazina ?
 
Kuna zingine unaambiwa na baadhi ya wahudumu wa mahakamani unabei gani ili tukupe dhamana ya NDG yako. Sanasana mahakama za mwanzo unafunguliwa droo unaambiwa weka humu kakae nje tutakuita. Hizo nazo zinaenda hazina ?
Hizo zinaishia mifukoni za hao wajanja
 
Asilimia 90 huwa ni katika maandishi tu.kama mtu akikwepa hiyo dhamana, mdhamini ataleta hiyo milioni 10. Mara chache sana mshtakiwa hutakiwa kuweka dhamana ya pesa taslimu hutokea kwenye kesi nzito
Kumbe mdhamini huwa hatoi hela? Na vipi akitoa na mshitakiwa akashinda kesi, hela inarudi?
 
Dhamana sio mapato mkuu, dhamana (kama ni fedha taslimu) hurudishwa kwa mhusika (mdhamini) baada ya kuisha kesi au muda wowote atakapoamua kujitoa kama mdhamini wa mtuhumiwa..itaingizwa kama mapato pale tu mtuhumiwa atakapokiuka masharti ya dhamana kwa kutoroka na mdhamini ashindwe kumfikisha mahakamani au kueleza mahali alipo ili asaidiwe kumpata...

Nashukuru namm nimepata jibu la dukuduku langu
 
Kumbe mdhamini huwa hatoi hela? Na vp akitoa na mshitakiwa akashinda kesi, hela inarudi?
sio mtuhumiwa kushinda kesi, bali kesi kuisha kwa ama mtuhumiwa kuhukumiwa kifungo, au faini au vyote viwili au kuachiwa huru. Vyovyote vile kesi itakavyoamuliwa.

Maana yake imefika mwisho na hivyo dhamana hata kama ni ya fedha lazima irudi kwa aliyeiweka (mdhamini) maana imekwishamaliza kazi yake ((kumdhamini mtuhumiwa wakati kesi inaendelea kusikilizwa), ni kama tu zitavyorudishwa hati za viwanja na mashamba kama ziliwekwa hizo.
 
Ni kwamba unasaini bond kuwa utawasilisha fedha hizo ikiwa uliemdhamini atatoroka hivyo hutoi pesa taslim lakini ikikulazimu kutoa pesa taslim unatakiwa upewe/ udai risiti ya fedha hizo ili dhamana inapokwisha urudishiwe mpunga wako.
Hili jibu ni sahihi na ndo ilivyo. Mleta mada kama hajalielewa basi afunge safari mpaka mahakama iliyo karibu yake kwa ufafanuzi zaidi.
 
Na ikitokea kwa mfano mshitakiwa akajiua vp hapo hela itarudishwa? Au akafariki katkati ya kesi
 
Na ikitokea kwa mfano mshitakiwa akajiua vp hapo hela itarudishwa? Au akafariki katkati ya kesi
Katika kesi ya jinai mtuhumiwa anapofariki, kesi huisha automatically , hivyo dhamana zitarudishwa
 
Hili jibu ni sahihi na ndo ilivyo. Mleta mada kama hajalielewa basi afunge safari mpaka mahakama iliyo karibu yake kwa ufafanuzi zaidi.
Mkuu usimdanganye jamaa, sio rahisi akapewa maelezo mahakamani, kwa mahakama zetu hizi !!, huwa hawapendi watu wajue haki zao wala sheria, kwani wakijua itakuwa ngumu kuwadhulumu au kuwaibia
 
Mkuu usimdanganye jamaa, sio rahisi akapewa maelezo mahakamani, kwa mahakama zetu hizi !!, huwa hawapendi watu wajue haki zao wala sheria, kwani wakijua itakuwa ngumu kuwadhulumu au kuwaibia
Nilimaanisha alichojibiwa kwenye post # 10 na aliyekazia kwenye post # 30 ni maelezo yanayompa jibu sahihi la swali lake. Nje ya hapo atadesa ndo nikashauri aende mahakamani. Ni kwa nia njema tu
 
sio mtuhumiwa kushinda kesi, bali kesi kuisha kwa ama mtuhumiwa kuhukumiwa kifungo, au faini au vyote viwili au kuachiwa huru. Vyovyote vile kesi itakavyoamuliwa, maana yake imefika mwisho na hivyo dhamana hata kama ni ya fedha lazima irudi kwa aliyeiweka (mdhamini) maana imekwishamaliza kazi yake ((kumdhamini mtuhumiwa wakati kesi inaendelea kusikilizwa), ni kama tu zitavyorudishwa hati za viwanja na mashamba kama ziliwekwa hizo.
Asante Mkuu kwa kunielewesha vema
 
Asilimia 90 huwa ni katika maandishi tu. kama mtu akikwepa hiyo dhamana, mdhamini ataleta hiyo milioni 10. Mara chache sana mshtakiwa hutakiwa kuweka dhamana ya pesa taslimu hutokea kwenye kesi nzito
Huwa zinakarabati majengo ya kota za police ili wapate kuwatumikia vzr[emoji23]
 
Dhamana sio mapato mkuu, dhamana (kama ni fedha taslimu) hurudishwa kwa mhusika (mdhamini) baada ya kuisha kesi au muda wowote atakapoamua kujitoa kama mdhamini wa mtuhumiwa, itaingizwa kama mapato pale tu mtuhumiwa atakapokiuka masharti ya dhamana kwa kutoroka na mdhamini ashindwe kumfikisha mahakamani au kueleza mahali alipo ili asaidiwe kumpata.

Hata hivyo mahakama itampa muda mtu huyu amtafute huyo mtuhumiwa na atakaposhindwa kumfikisha mahakamani mpaka muda aliopewa kuisha..basi ndio watakapoichukua hiyo pesa (kutaifisha) na kama dhamana ni mali (nyumba au kiwanja) watavutaifisha na kuvipiga mnada
Baada ya kuchukua hizo fedha huenda wapi?
 
Back
Top Bottom