Fedha za dhamana zitolewazo mahakamani huwa zinaenda wapi?

Naomba kuuliza, kama umemdhamini mtu mahakama ya Mwanzo amepangiwa tarehe ya kurudi Mahakamani, ikifika tareh husika kwani ni lazima mdhamini uwepo au yey mtuhumiwa akienda si basi inatosha?

Au??
mkuu hili swali lilikuwa nje ya uwezo wangu, ila nashukuru mchanguaji hapo juu ametoa ufafanuzi
 
Kuna zingine unaambiwa na baadhi ya wahudumu wa mahakamani unabei gani ili tukupe dhamana ya ndugu yako. Sanasana Mahakama za Mwanzo unafunguliwa droo unaambiwa weka humu kakae nje tutakuita. Hizo nazo zinaenda hazina ?
 
Kuna zingine unaambiwa na baadhi ya wahudumu wa mahakamani unabei gani ili tukupe dhamana ya NDG yako. Sanasana mahakama za mwanzo unafunguliwa droo unaambiwa weka humu kakae nje tutakuita. Hizo nazo zinaenda hazina ?
Hizo zinaishia mifukoni za hao wajanja
 
Asilimia 90 huwa ni katika maandishi tu.kama mtu akikwepa hiyo dhamana, mdhamini ataleta hiyo milioni 10. Mara chache sana mshtakiwa hutakiwa kuweka dhamana ya pesa taslimu hutokea kwenye kesi nzito
Kumbe mdhamini huwa hatoi hela? Na vipi akitoa na mshitakiwa akashinda kesi, hela inarudi?
 

Nashukuru namm nimepata jibu la dukuduku langu
 
Kumbe mdhamini huwa hatoi hela? Na vp akitoa na mshitakiwa akashinda kesi, hela inarudi?
sio mtuhumiwa kushinda kesi, bali kesi kuisha kwa ama mtuhumiwa kuhukumiwa kifungo, au faini au vyote viwili au kuachiwa huru. Vyovyote vile kesi itakavyoamuliwa.

Maana yake imefika mwisho na hivyo dhamana hata kama ni ya fedha lazima irudi kwa aliyeiweka (mdhamini) maana imekwishamaliza kazi yake ((kumdhamini mtuhumiwa wakati kesi inaendelea kusikilizwa), ni kama tu zitavyorudishwa hati za viwanja na mashamba kama ziliwekwa hizo.
 
Ni kwamba unasaini bond kuwa utawasilisha fedha hizo ikiwa uliemdhamini atatoroka hivyo hutoi pesa taslim lakini ikikulazimu kutoa pesa taslim unatakiwa upewe/ udai risiti ya fedha hizo ili dhamana inapokwisha urudishiwe mpunga wako.
Hili jibu ni sahihi na ndo ilivyo. Mleta mada kama hajalielewa basi afunge safari mpaka mahakama iliyo karibu yake kwa ufafanuzi zaidi.
 
Na ikitokea kwa mfano mshitakiwa akajiua vp hapo hela itarudishwa? Au akafariki katkati ya kesi
 
Na ikitokea kwa mfano mshitakiwa akajiua vp hapo hela itarudishwa? Au akafariki katkati ya kesi
Katika kesi ya jinai mtuhumiwa anapofariki, kesi huisha automatically , hivyo dhamana zitarudishwa
 
Hili jibu ni sahihi na ndo ilivyo. Mleta mada kama hajalielewa basi afunge safari mpaka mahakama iliyo karibu yake kwa ufafanuzi zaidi.
Mkuu usimdanganye jamaa, sio rahisi akapewa maelezo mahakamani, kwa mahakama zetu hizi !!, huwa hawapendi watu wajue haki zao wala sheria, kwani wakijua itakuwa ngumu kuwadhulumu au kuwaibia
 
Mkuu usimdanganye jamaa, sio rahisi akapewa maelezo mahakamani, kwa mahakama zetu hizi !!, huwa hawapendi watu wajue haki zao wala sheria, kwani wakijua itakuwa ngumu kuwadhulumu au kuwaibia
Nilimaanisha alichojibiwa kwenye post # 10 na aliyekazia kwenye post # 30 ni maelezo yanayompa jibu sahihi la swali lake. Nje ya hapo atadesa ndo nikashauri aende mahakamani. Ni kwa nia njema tu
 
Asante Mkuu kwa kunielewesha vema
 
Asilimia 90 huwa ni katika maandishi tu. kama mtu akikwepa hiyo dhamana, mdhamini ataleta hiyo milioni 10. Mara chache sana mshtakiwa hutakiwa kuweka dhamana ya pesa taslimu hutokea kwenye kesi nzito
Huwa zinakarabati majengo ya kota za police ili wapate kuwatumikia vzr[emoji23]
 
Baada ya kuchukua hizo fedha huenda wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…