Habari za muda naomba utusaidie kupasa sauti kwa kweli Halmashauri yetu ya Chato hawajatutendea haki sisi walimu wa sekondari tulioajiriwa Mwaka 2025.
Walitupa fedha za kujikimu shilingi laki moja tu, walitulipa 27 Aprili 2026, kwanini sisi tumepewa fedha kidogo angali wenzetu wa Shule ya Msingi walilipwa mapema na fedha yao ilikuwa nyingi kiasi?
Tumefanya jitihada nyingi sana kwenda halmashauri kila tukienda mara fedha hazifika, zikifika tutaingiziwa sasa wameamua kutuingizia laki.
Kwa kweli inaumiza sana, ukizingatia tunafanyakazi katika katika mazingira magumu, bado pesa wanakulipa kama sadaka wakati ni haki ya mtumishi.
Naomba utupasie sauti halmashauri ya Chato, wanatuonea sana, na fedha hizo wanaingiza kama malipo ya likizo wakati bado hatuna sifa za kulipwa likizo bado, naomba utupazie sauti tafadhali.
Ilikuwa na haja gani kutulipa laki kama hakuna fungu si wangeendelea kutucheleweshea tu kutulipa kuliko kutuweka laki moja kwa usawa huu wa maisha laki ni nini jamani?
Malipo yanapaswa kuanzia laki 9 na saivi uchumi umekuwa hata milioni ndiyo ilitakiwa tupate.
Halmashauri Nyingi Zina Uzandiki,,,Chuki,,,Unafki,,,Roho Mbaya,,Njaa Za Hovyo,,,Upuuzi,,Ujuaji Wa Kipumbavu,,Low Minded People,,,Wivu,,Kujipendekezapendekeza,,Usaliti.....n.k,n.k.....