JOSE KASANO
Senior Member
- Apr 23, 2013
- 122
- 95
Ni jambo la kustaajabu kuwa tangu kuripoti katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba mkoani Kagera tarehe1.04.2014 hadi leo hii walimu wapya hatujalipwa fedha yoyote na uongozi wa manispaa. Wametuzungusha sana kwamba tuandike barua za madai, tumeziandika lakini wanasema bado wanaendelea kuzikagua.
Leo tarehe 3.04.2014 wamewaita wakuu wa shule za sekondari na kutukabidhi kwao kwa maana ya kwamba wao ndio waangalie utaratibu wa kutupa hifadhi hadi hapo tutakapolipwa jambo liliibua manunguniko makubwa sana na wakuu wa shule hadi wengine kusema kuwa ni bora serikali isingewaleta walimu wapya katika manispaa hiyo kama fedha za kuwalipa hazijakamilika.
''Kimsingi huu mzigo sisi kama wakuu wa shule hatuuwezi, kama serikali imeshindwa sembuse sisi amabo hatuna mafungu ya kulipa dharula za namna hii'' amesema mkuu wa shule mojawapo katika manispaa ya Bukoba.
Walimu wapya tuliopangwa katika manispaa hii tumefikia hatua ya kukata tamaa ya kwenda kufanya kazi kutokana na hali ya ukaribisho na uwezeshwaji tulioupata katika manispaa hii. Mkurugenzi hatujamuona isipokuwa wawakilishi wake ambao nao wanakosa majibu sahihi, Ofisa elimu wa sekondari Bwana Rumanyika anaonekana kutokuwa na wasiwasi na hali hii inayoendelea. Tumeambiwa turudi kesho Ijumaa ili kuona mchakato umefikia wapi.Siasa tu hapa ndiyo inafanya kazi.Tumetumia kiasi chote cha pesa tulichokuja nacho maana kulala nyumba za wageni chumba hakipungui elfu kumi (10,000=), chakula hapa ni gharama kwa maana chakula cha kushiba hakipungui 5,000/=, shule nyingi hapa mjini hazina nyumba za walimu hivyo walimu lazima kupanga uraiani.Mambo yote haya yanahitaji fedha ambayo tulitakiwa tuwe tumeliwa kama halmashauri zingine hapa nchini zilivyofanya.
Tafadhali wizara ya TAMISEMI na ELIMU walishughulikie TATIZO hili haraka kuwafanya walimu wapya wa manispaa ya Bukoba kurudisha ari ya kwenda vituoni kufanya kazi kwa moyo mweupe