A
Anonymous
Guest
Nikiwa mmoja wa waajiriwa wapya kupitia Ajira Mpya, na napenda kueleza changamoto kubwa tunayoipitia kuhusu fedha za kujikimu.
Kwenye baadhi ya halmashauri, inaelezwa kuwa fedha hizi zinafika mapema kabisa, lakini kinachotokea ni kwamba zinachelewa kuwafikia wahusika. Hata zinapofika, hazitolewi kwa wakati au zinatolewa kwa awamu—unapewa kiasi kidogo ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya kuanza maisha mapya ya kazi.
Kuna baadhi ya wenzetu hadi sasa hawajapata kabisa fedha hizo, licha ya kuwa ni haki yao ya msingi kama waajiriwa wapya. Hali hii inatupa wakati mgumu sana, hasa ukizingatia wengi wetu tumeanza kazi katika maeneo mapya bila maandalizi ya kifedha ya kutosha.
Kwa hali ilivyo sasa, inaonekana kuna changamoto katika mfumo wa utoaji wa fedha hizi kupitia halmashauri, jambo linalosababisha ucheleweshaji au kutotolewa kwa kiwango kinachostahili.
Soma Pia: Sisi walimu wa ajira mpya 2026 Halmashauri ya mji Newala - Mtwara hatujalipwa fedha za kujikimu. Mamlaka husika zipo kimya mpaka sasa
Ningeshauri kwa heshima kubwa kwa TAMISEMI, Wizara na Serikali kwa ujumla, kuwe na utaratibu wa fedha za kujikimu kuwekwa moja kwa moja kwenye akaunti za waajiriwa wapya. Hii itasaidia kuondoa ucheleweshaji, utoaji wa fedha kwa awamu, na hata uwezekano wa baadhi ya watu kukosa kabisa haki zao.
Tunaomba mamlaka husika zituangalie kwa jicho la huruma na kuchukua hatua ili kuhakikisha kila mwajiriwa mpya anapata stahiki zake kwa wakati na kwa ukamilifu.