#COVID19 Fedha za kupambana na UVIKO19: Tenda ya Sept 29 na mwisho wa maombi Sept 30?

#COVID19 Fedha za kupambana na UVIKO19: Tenda ya Sept 29 na mwisho wa maombi Sept 30?

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mapema leo Rais Samia akiwaapisha viongozi mbalimbali ameeleza wazi kuwa hatovumilia viongozi wala RUSHWA. Hata Siku ya Jumapili wakati akizindua mpango wa Serikali wa kuinua uchumi na kukabiliana na UVIKO19 alisisitiza matumizi sahihi ya fedha za hizo huku akiwataka wasimamizi kuzingatia sheria na kanuni zote za matumizi.

Habari mbaya ni kwamba, inawezekana Wizara ya Afya ikawa wameshayakoroga maji mapema kabisa katika kutangaza tenda kwani ni dhahiri kuna watu wamekula "dili" wakapeana tenda juu kwa juu na barua ya tenda imetolewa tu kama ushahidi. Kwa mujibu wa barua hiyo (Iko hapo chini), wizara ya afya imetangaza tenda tarehe 29/09/2021. Lakini sharti la 7 inawataka waombaji wote kuwasilisha nyaraka zao halisi tarehe 30/09/2021 kabla ya saa nane mchana. Kwa lugha rahisi mwombaji anatakiwa kujaza nyaraka na kuzifikisha Dodoma katika muda chini ya masaa 24. Hii ni wazi kuna watu wamepeana dili hapa na Rais Samia anapaswa kuanza kushughulika na hawa watu mapema iwezekanavyo

Afya.jpeg

Soma ufafanuzi wa Wizara: #COVID19 - Serikali yakana kuwepo upendeleo au rushwa kwenye kampeni ya kuhamasisha chanjo
 
Kama muhusika ni muhusika, nini kitatokea?
 
Ndicho walichokuwa wanakitaka Chadema na gaidi wao
 
Kutoka 23: 8

Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.
 
Mbona mie nimesikia hiyo kitu ilishafutwa na wizara ... ??????
 
Kutoka 23: 8

Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.
Shekh hii ulikuwa enzi ya utawala wa Nabkodonosoro, kwa hali ilivyongumu mmgh macho hayapofuki mkuu ahahah
 
Shekh hii ulikuwa enzi ya utawala wa Nabkodonosoro, kwa hali ilivyongumu mmgh macho hayapofuki mkuu ahahah

Mithali 21: 13-14
Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa. Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.
 
Tulia wewe hizi ni zile tenda za "wenyewe" unakuta bidder anaandaa tangazo, criteria zote za selection, na proposal inakuwa imeshaandaliwa pamoja na bidding documents kabla ya tenda kutangazwa🐒
 
Shekh hii ulikuwa enzi ya utawala wa Nabkodonosoro, kwa hali ilivyongumu mmgh macho hayapofuki mkuu ahahah

Mithali 21: 13-14
Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa. Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.
 
Hizi pesa zitapigwa sana watu ni wataalamu sana wakupiga pesa na report zitakua clean. Imagine jana tu ule ufunguzi ukifanya coast analysis utajikuta tumetumia bilion 1. maperdiem, fuel, nk.
 
Mama keshasema utaratibu wa tenda utatuchelewesha, kwa hiyo tarajia ujanja ujanja wa kupeana michongo kwa wakubwa......sisi wanyonge tuendelee kuchangia tozo.
 
Mithali 21: 13-14
Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa. Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.
Rushwa inaudhi kwani inanyima watu haki zao za Msingi,lkn mala rushwa ndo yanatamba mjini.

Rushwa ina aina nyingi,mfano watu wanakopa World Bank lkn....
 
Naona umeicopy kama ilivyo kutoka kwa Activist Dr Feva Lwaitama. Plagiarism hiyo mkubwa.
 
Back
Top Bottom