Tamu3
Member
- Feb 17, 2023
- 28
- 18
FEDHA ZA MAUZAUZA
1.
Tulikuwa kijiweni, tukizogoa zogoa,
Umbeya tukipigieni, tukiyapisha masaa,
Bia tamu tukinyweni, pia soka kichambua,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
2.
Mara mtu akapita, shanga nyingi zi shingoni,
Kati yetu akamwita, machache kiulizweni,
Akaja bila kusita, karibu akaketini,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
3.
Mengi lituelezea, nilianza kuvutiwa,
Mfuko akafungua, kipeperushi katowa,
Akadai anatoa, utajiri anagawa,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
4.
Nilikuwa namba wani, kuomba kutajirika,
Nilikuwa natamani, fedha nyingi kuzishika,
Namba tukapeaneni, akaanza kuondoka,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
5
Asubuhi kesho yake, kwake nikamuendea,
Akanipokea mke, kigodani nikakaa,
Nikakuta nyumba yake, ipo karibu na njia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
6
Mganga akarejea, kusaka dawa porini,
Ngozi ya chui mevaa, na mkia mkononi,
Salamu akazitoa, shida nikamwelezeni,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
7.
Kibuyu akachukua, akaanza kuongea,
Lugha nisiyoijua, aliongea ongea,
Nikaombwa kusogea, kibuyu linipatia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
8.
Sema yote utakayo, mganga niliambia,
Chafya nyingi pia myayo, nikaanza kuzitoa,
Akazogezea kiyo, ndugu mule katokea,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
9.
Nikaletewa sindano, yenye ncha Kali Sana,
Ikifanana na jino, moyo ukagunaguna,
Wangu kushoto mkono, liamuriwa kubana,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
10.
Bila huruma kabisa, ndugu yangu nikachoma,
Kioo nilipogusa, pakawa panalalama,
Mganga akaniasa, pesa nyingi nitachuma,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
11.
Nyumbani nikarejea, nikakaa siku mbili,
Msiba ukatokea, wenye vilio vikali,
Huzuni ilitopea, wiki zaidi ya mbili,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
12
Mwaka sasa ukapita, magari nikanunua,
Ghorofa kumi sita, mjini zimechanua,
Heshima nikaipata, nitakacho najilia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
13.
Dukani kukasheheni, hizo za gari spea,
Ndugu toka kijijini, kwangu nao lihamia,
Sote tulifurahini, maisha yakiwa murua,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
14
Ba'da ya myaka kupita, mganga lipiga simu,
Lisema bila kusita, akasema jambo gumu,
Masharti sijafwata, utajiri haudumu,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
15
mganga limulilia, msamaha hakutoa,
Simu alinikatia, hewani akapotea,
Nililia na kulia, mawazo menizidia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
16.
Hofu nyingi linishika, usiku siwezi lala,
Kutwa nashinda mechoka, Chakula siwezi kula,
Nilimtafuta kaka, aniombee kwa Mola,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
17.
Siku moja lisafiri, mali kienda kufunga,
Tuliondoka vizuri, mfukoni nina kanga,
Katikati ya safari, gari mti likagonga,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
18.
Watu wote walipona, mie ndie livunjika,
Mguu nikawa sina, gotini ukakatika,
Lichopanda nikavuna, maisha liharibika,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
19.
Safari nikasitisha, ajali lipotokea,
Nilishuka kimaisha, mali zote lipotea,
Na ndugu liniwachosha, wote ndugu lipotea,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
20.
Kwa mganga lirejea, matatizo kutatua,
Kioja nilishangaa, wadai aliugua,
Alikwishakujifia, kaburini meozea,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
21.
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu,
Bavu langu limeoza, malipo kwayo maovu,
Jamii ninaijuza, jitoe kwenye maovu,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
22.
Tafuta Mali halali, kwa mganga sio dili,
Kule Kuna pilipili, machoni zina ukali,
Mali zisizo halali, taharibu wako mwili,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa Mashairi na ngano za Kiafrika
MUFINDI TANZANIA
1.
Tulikuwa kijiweni, tukizogoa zogoa,
Umbeya tukipigieni, tukiyapisha masaa,
Bia tamu tukinyweni, pia soka kichambua,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
2.
Mara mtu akapita, shanga nyingi zi shingoni,
Kati yetu akamwita, machache kiulizweni,
Akaja bila kusita, karibu akaketini,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
3.
Mengi lituelezea, nilianza kuvutiwa,
Mfuko akafungua, kipeperushi katowa,
Akadai anatoa, utajiri anagawa,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
4.
Nilikuwa namba wani, kuomba kutajirika,
Nilikuwa natamani, fedha nyingi kuzishika,
Namba tukapeaneni, akaanza kuondoka,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
5
Asubuhi kesho yake, kwake nikamuendea,
Akanipokea mke, kigodani nikakaa,
Nikakuta nyumba yake, ipo karibu na njia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
6
Mganga akarejea, kusaka dawa porini,
Ngozi ya chui mevaa, na mkia mkononi,
Salamu akazitoa, shida nikamwelezeni,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
7.
Kibuyu akachukua, akaanza kuongea,
Lugha nisiyoijua, aliongea ongea,
Nikaombwa kusogea, kibuyu linipatia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
8.
Sema yote utakayo, mganga niliambia,
Chafya nyingi pia myayo, nikaanza kuzitoa,
Akazogezea kiyo, ndugu mule katokea,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
9.
Nikaletewa sindano, yenye ncha Kali Sana,
Ikifanana na jino, moyo ukagunaguna,
Wangu kushoto mkono, liamuriwa kubana,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
10.
Bila huruma kabisa, ndugu yangu nikachoma,
Kioo nilipogusa, pakawa panalalama,
Mganga akaniasa, pesa nyingi nitachuma,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
11.
Nyumbani nikarejea, nikakaa siku mbili,
Msiba ukatokea, wenye vilio vikali,
Huzuni ilitopea, wiki zaidi ya mbili,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
12
Mwaka sasa ukapita, magari nikanunua,
Ghorofa kumi sita, mjini zimechanua,
Heshima nikaipata, nitakacho najilia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
13.
Dukani kukasheheni, hizo za gari spea,
Ndugu toka kijijini, kwangu nao lihamia,
Sote tulifurahini, maisha yakiwa murua,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
14
Ba'da ya myaka kupita, mganga lipiga simu,
Lisema bila kusita, akasema jambo gumu,
Masharti sijafwata, utajiri haudumu,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
15
mganga limulilia, msamaha hakutoa,
Simu alinikatia, hewani akapotea,
Nililia na kulia, mawazo menizidia,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
16.
Hofu nyingi linishika, usiku siwezi lala,
Kutwa nashinda mechoka, Chakula siwezi kula,
Nilimtafuta kaka, aniombee kwa Mola,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
17.
Siku moja lisafiri, mali kienda kufunga,
Tuliondoka vizuri, mfukoni nina kanga,
Katikati ya safari, gari mti likagonga,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
18.
Watu wote walipona, mie ndie livunjika,
Mguu nikawa sina, gotini ukakatika,
Lichopanda nikavuna, maisha liharibika,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
19.
Safari nikasitisha, ajali lipotokea,
Nilishuka kimaisha, mali zote lipotea,
Na ndugu liniwachosha, wote ndugu lipotea,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
20.
Kwa mganga lirejea, matatizo kutatua,
Kioja nilishangaa, wadai aliugua,
Alikwishakujifia, kaburini meozea,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
21.
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu,
Bavu langu limeoza, malipo kwayo maovu,
Jamii ninaijuza, jitoe kwenye maovu,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
22.
Tafuta Mali halali, kwa mganga sio dili,
Kule Kuna pilipili, machoni zina ukali,
Mali zisizo halali, taharibu wako mwili,
Fedha za mauzauza, menitia ulemavu.
Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa Mashairi na ngano za Kiafrika
MUFINDI TANZANIA