SI KWELI Fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Jimbo la Hai Kilimanjaro hazionekani Jimboni tangu 2020-2022

SI KWELI Fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Jimbo la Hai Kilimanjaro hazionekani Jimboni tangu 2020-2022

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
MADAI
Yapo madai kuwa Fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Jimbo la Hai Kilimanjaro hazionekani Jimboni tangu 2020-2022. Mbunge wa Jimbo la Hai, unaulizwa Fedha Za mfuko wa jimbo kwa Jimbo la Hai zimeweza kusaidia shughuli gani tangu 2020 hadi 2022?

Aidha, inadaiwa kuna kila dalili fedha hizo wanalamba asali wachache. Miaka ya 2015-2020 fedha hizo zilioneka jimboni na Kufanya shughuli muhimu ila kwa sasa mbunge anajengea nyumba yake ya kuishi.

1667862898813.png

1667862934038.png

1667862974022.png
 
Tunachokijua
Yemeibuka madai kuwa Fedha za mfuko wa Jimbo la Hai Kilimanjaro hazionekani madai hayo yaliibuka mnamo Agosti 7, 2022 yakiletwa na Mwanachama wa JamiiForums anayeitwa Peno Hosegawa aliyeleta aniko lenye Kichwa Fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Jimbo la Hai Kilimanjaro hazionekani. Sehemu ya andiko hilo linadai kwamba:

Mbunge wa Jimbo la Hai, unaulizwa Fedha Za mfuko wa jimbo kwa Jimbo la Hai zimeweza kusaidia shughuli gani tangu 2020 hadi 2022? Kuna kila dalili fedha hizo wanalamba asali wachache.
Miaka ya 2015-2020 fedha hizo zilioneka jimboni na Kufanya shughuli muhimu ila kwa sasa mbunge anajengea nyumba yake ya kuishi.

Hata hivyo, madai haya hayajaelezewa kwa kina zaidi na hakuna chanzo kingine kilichoripoti kuwapo kwa wizi wa fedha za mfuko wa Jimbo la Hai.

Upi ukweli wa madai hayo?
JamiiForums imefanya mawasiliano na Mbunge wa Hai Saasisha Mafue ambaye amekanushauvumi huo na kudai kuwa hakuna ukweli kwenye jambo hilo. Akifafanua zaidi hoja yake Mbunge Saasisha Mafue anasema:

“Fedha hizo zipo kwa mujibu wa Sheria, haziingii kwenye akaunti ya Mbunge kama wengi wanavyodhani, zinaingia katika akaunti ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
“Zikiingia Mkurugenzi anamtaarifu Mbunge kama Mwneykiti wa Mfuko wa Jimbo ambaye anaitisha kikao kwa ajili ya maelekezo, fedha hizo zinaenda kwenye miradi ya Serikali.
“Mimi huwa huwa ninaita Madiwani tunajadili kuhusu miradi na kuidhinisha, lakini wanaonunua, wanaosambaza, wanaosimamia ni Halmashauri na siyo mimi Mbunge.”

Ametaja Wajumbe wa Mfuko wa Jimbo kuwa ni:
1. Saashisha E. Mafuwe (Mb)- Mwenyekiti
2. Leonard Luhwavi - Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na uratibu -Katibu.
3. Judica J. Munisi - Diwani wa Machane Kaskazin -Mjumbe
4. Zanika A. Mushi Diwani V/Maalum-Mjumbe.
5. Hellen J. Munuo- Mtendaji Kata ya Muungano-Mjumbe.
6. Andrew E. Msuya - Mtendaji Kata ya Masama Mashar - Mjumbe.
7. Asifiwe James Malya - Mwakilishi kutoka NGO

Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo wa kina ambao Mbenge Mafue ameutoa sambamba na kutoa andiko rasmi kuelezea kwa kina, JamiiForums tunaona kuwa madai yaliyoibuliwa kuwa fedha za mfuko wa jimbo la Hai Kilimanjaro hazionekani, yanakosa mashiko.
Back
Top Bottom