Fedha za Mfuko wa Jimbo Zaelekezwa kwenye Ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi

Fedha za Mfuko wa Jimbo Zaelekezwa kwenye Ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini umepokea Tsh 75,796,000 (Tsh 75.8m) na fedha zote hizo zimeelekezwa kwenye ujenzi na ukamilishaji wa Maabara za Masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia & Bailojia) kwenye Sekondari za Kata za Musoma Vijijini.

Lengo letu la sasa ni Musoma Vijijini kuwa na High Schools 4-6 za Masomo ya Sayansi ndani ya miaka mitatu ijayo.

Jimbo letu lenye Kata 21, lina jumla ya Sekondari 27. Kati ya hizo, 25 ni za Kata/Serikali na 2 ni za madhehebu ya Dini (Katoliki & Sabato).

Leo, Ijumaa, tarehe 17.3.2023, Mwenyekiti wa Mfuko wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo (Mb) ameongoza Kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichogawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko huo.

Fedha za Mfuko huo zimetunzwa na Halmashauri yetu (Musoma DC) na ndiyo itakayofanya manunuzi ya vifaa vya ujenzi.

Wakuu wa Shule za Sekondari zetu zote za Kata (25) wamekaribishwa kwenye Kikao hicho.

VIFAA VYA UJENZI VITAKAVYONUNULIWA

*Jumla ya Fedha:
Tsh 75,796,000
*Saruji Mifuko (50%)
1,613
*Mabati (40%)
947
*Nondo (10%)
337

VIGEZO VYA MGAO
*Sekondari mpya zimepewa kipaumbele
*Sekondari zisizo kwenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha zimepewa kipaumbele

*Sekondari zilizoshindwa kutumia vifaa vilivyogawiwa huko nyuma havikugawiwa cho chote.
*Sekondari ambazo wizi umefanyika hazikugawiwa cho chote.

MGAO WA VIFAA VYA UJENZI

(1) SARUJI MIFUKO
*Muhoji (300)
*Bwai (300)
*Mkirira (200)
*Mabui (200)
*Mtiro (200)
*Bukima (150)
*Bulinga (150)
*Ifulifu (100)

(2) MABATI Gauge 28
*Seka (142)
*Kigera (112)
*Muhoji (110)
*Bwai (110)
*Busambara (104)
*Bukwaya (100)
*Mabui (92)
*Suguti (62)
*Bukima (62)
*Makojo (50)

(3) NONDO mm12
*Muhoji (50)
*Bwai (50)
*Seka (50)
*Busambara (50)
*Mtiro (49)
*Kigera (48)
*Bukwaya (40)

Kikao cha ugawaji wa vifaa hivyo hapo juu kimefanyika kwenye Ofisi za Muda za Halmashauri yetu zilizoko Kijijini Nyang'oma, Kata ya Mugango

UPOKEAJI NA USAFIRISHAJI WA VIFAA VYA UJENZI

Alhamisi, tarehe 23.3.2023, Wakuu wa Shule za Sekondari na Bodi zao watasafirisha vifaa vya ujenzi walivyogawiwa kutoka Bohari ya Halmashauri yetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Ijumaa, 17.3.2023
spmnjhu.JPG
 
Back
Top Bottom